Friday, September 28, 2012

STR8MUZIK FREESTYLE ILIVYOBAMBA

1.Dancers
Mmoja wa wanakundi cha waburudishaji cha BFB cha mkoani Mwanza akifanya vitu vyake katika mpambano wa kusaka ma-MCs na DJs wa STR8MUZIK Freestyle 2012 mkoani mwanza uliofanyika katika ukumbi wa Stone mjini humo jana usiku.(Picha ya Excutive Solutions)
2.Kabebwa JUU
Mashabiki wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza wakiwa wamembeba juu MC bora wa mwaka mkoani humo Joash Magadula katika mpambano uliofanyika jana usiku katika ukumbi wa Stone mjini humo.(Picha ya Executive Solutions)
3. DJ Winner
Mshindi wa mpambano wa ma-DJ wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani mwanza DJ Juma Ramadhani(Kati) akitumbuiza mara baada ya kukabidhiwa chombo cha kupigishia muziki chenye thmani ya Sh mil 7 na Meneja wa TCC Mkoa wa Mwanza Deogratius Kamugisha(Kulia), huku mshindi wa upande wa ma-MC mkoani humo Joash Magadula akishuhudia na zawadi yake mkononi.(Picha ya Executive Solutions)
4.MC Winner
Meneja wa TCC Mkoani Mwanza Deogratius Kamugisha akimkabishi tuzo MC bora wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza Joash Magadula katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Stone mjini humo jana.(Picha ya Executive Solutions)
5.Mashabiki 1,2
Umati wa wana-Mwanza ulivyoshona katika ukumbi Club Stone mjini humo katika mpambano wa STR8MUZIK 2012 FreeStyle Mwanza.(Picha ya Executive Solutions)
6.Easy Business
Msanii wa kizazi kipya Easy Business ambaye ni maarufu kwa kibao chake cha “Ongea na Mshua” akitumbuiza katika mpabano wa STR8MUZIK 2012 FreeStyle Mwanza
7.Washindi Wote
Meneja wa TCC tawi la Mwanza, Bw Deogratius Kamugisha (Katikati) akipozi na washindi wa mpambano wa ma MCs na DJs STR8MUZIK Freetyle 2012 mkoani mwanza. Kutoka kushoto ni Mshindi wa pili wa DJs Ruyobya Johannes a.k.a DJ Yt,Mshindi wa kwanza kwa DJs Juma Ramadhani,Msindi wa Pili katika kategori ya ma-MCs Nchana Antony na Mshindi wa MCs Joash Magadula a.k.a MC Magadash.(Picha ya Executive Solutions)








Picha na bin zubeiry

No comments:

Post a Comment