.
Kaimu mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa mara dr joseph nyamagwira akitoa takwimu kwa waandishi wa habari za watu waliofariki dunia na waliojeruhiwa . |
mkuu wa wilaya ya musoma jackson msome akiwapa pole ndugu wa majeruhi na waliopoteza maisha. |
Watu 13 wamefariki dunia kwa ajali ya basi dogo la abiria aina ya hiace na wengine 18 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa mara kwa matibabu zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara Dokta Joseph nyamagwira amesema kuwa watu 10 walifariki papo hapo baada ya gari hiyo kupasuka tairi la nyuma na kupoteza mwelekeo na hatimaye kupinduka mara tatu na kupoteza maisha ya wananchi.
Nyamagwira alisema watu watatu waliokuwa majeruhiwa walifariki dunia mara baada ya kufikishwa hospitali wanaume wawili na mwanamke mmoja ,majeruhiwa wa kiume mmoja alikuwa na majeraha makubwa kichwani na mwingine alipasuka vandama na mwanamke alivunjika mbavu.
Alisema kuwa juhudi za kuwatibu Majeruhiwa zianaendelea vizur kwa ushirikiano wa madaktar,i isipokuwa majeruhiwa mmoja aliyevunjika mguu amepelekwa katika hospitali ya rufaa ya bugando kwaajili ya kuwekewa chuma ili aweze kupona haraka.
Gari hilo lilikuwa likitoka Musoma Mjini kuelekea butiama na ajali hiyo ilitokea eneo la nyabange nje kidogo ya manispaa ya musoma majira ya saa kumi na mbili jioni.
Mkuu wa wilaya ya musoma Jackson msome amewatembelea majeruhi wa ajali hiyo leo na kuwahakikishia ndugu wa majeruhi kuwa serikali iko pamoja nao na serikali inahakikisha huduma zote muhimu za matibabu zinapatikana hospitalini hapo ili waweze kupona.
No comments:
Post a Comment