Kamanda wa polisi wa mkoa wa mara Absalom mwakyoma akitoa taarifa ya kifo mbele ya waandishi wa habari. |
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha ketasakwa wilayani butiama amefariki dunia akikimbizwa katika kituo cha afya kiagata kufuatia kupigwa na kitu kizito kichwani .
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa mara Absalom Mwakyoma alisema kuwa mnamo 29 agosti 2012 majira ya saa moja usiku katika kijiji cha ketasakwa ,kata ya bwiregi ,tarafa ya kiagata wilayani butiama mkoani mara, amemtaja marehemu maswe 26 alijeruhiwa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na Shera wasaga ,ambapo ugomvi huo ulitokea katika klabu cha pombe za kienyeji.
Baada ya kupigwa kitu kizito kichwani juhudi zilifanyika za kupelekwa katika kituo cha afya kiagata kwa matibabu lakini alifariki dunia .
Mwakyoma alisema kuwa mtuhumiwa alitoroka baada ya tukio hilo na jitihada za kumtafuta na hatimaye kumfikisha mahakamani zinaendelea.
Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa mazishi.
Kamanda ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kuepukana na ulevi wa kupindukia.
No comments:
Post a Comment