Monday, September 10, 2012

kichekesho

Sharo alikuwa ndo kwaaaaaaanza kafanikiwa kupata mkoko wake mpya baada ya kutoa visingle vyake viwili witatu, akawa na hamu kweli aende nalo Leaders akawakoge masister duuuh nini...Wakati akizubaazubaa mtaani kwake mlango wa gari ukiwa wazi daladala moja likapita na kuuzoa mlango, Sharo akawa anapiga kelele....
"Oooh my GAD... Gari langu men, daladala imeharibu gari langu meeeen..."
Trafiki alipofika akamkuta Sharo bado analalamika kuhusu ule mlango. Trafiki akamwambia, "Hivi kwanini unajali mali namna hii? Mbona hulalamiki mkono wako wote wa kushoto ngozi imechubuka?!?" Sharo ndo akagundua kumbe daladala lilimkwangua ngozi mkono mzima, baada ya kujicheki fresh akapiga kelele zaidi,
"Oh Mamaa, saa yangu men...."

No comments:

Post a Comment