STR8MUZIK FREESTYLE ILIVYOBAMBA
1.Dancers
Mmoja
wa wanakundi cha waburudishaji cha BFB cha mkoani Mwanza akifanya vitu vyake
katika mpambano wa kusaka ma-MCs na DJs wa STR8MUZIK Freestyle 2012 mkoani
mwanza uliofanyika katika ukumbi wa Stone mjini humo jana usiku.(Picha ya Excutive
Solutions)
2.Kabebwa JUU
Mashabiki wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani
Mwanza wakiwa wamembeba juu MC bora wa mwaka mkoani humo Joash Magadula katika
mpambano uliofanyika jana usiku katika ukumbi wa Stone mjini humo.(Picha ya
Executive Solutions)
3. DJ Winner
Mshindi
wa mpambano wa ma-DJ wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani mwanza DJ Juma
Ramadhani(Kati) akitumbuiza mara baada ya kukabidhiwa chombo cha kupigishia
muziki chenye thmani ya Sh mil 7 na Meneja wa TCC Mkoa wa Mwanza Deogratius
Kamugisha(Kulia), huku mshindi wa upande wa ma-MC mkoani humo Joash Magadula
akishuhudia na zawadi yake mkononi.(Picha ya Executive Solutions)
4.MC Winner
Meneja wa TCC Mkoani Mwanza Deogratius
Kamugisha akimkabishi tuzo MC bora wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza Joash
Magadula katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Stone mjini humo
jana.(Picha ya Executive Solutions)
5.Mashabiki 1,2
Umati wa wana-Mwanza ulivyoshona katika ukumbi
Club Stone mjini humo katika mpambano wa STR8MUZIK 2012 FreeStyle Mwanza.(Picha
ya Executive Solutions)
6.Easy Business
Msanii wa kizazi kipya Easy Business ambaye ni
maarufu kwa kibao chake cha “Ongea na Mshua” akitumbuiza katika mpabano wa
STR8MUZIK 2012 FreeStyle Mwanza
7.Washindi Wote
Meneja wa TCC tawi la Mwanza, Bw Deogratius Kamugisha (Katikati) akipozi
na washindi wa mpambano wa ma MCs na DJs STR8MUZIK Freetyle 2012 mkoani mwanza.
Kutoka kushoto ni Mshindi wa pili wa DJs Ruyobya Johannes a.k.a DJ Yt,Mshindi
wa kwanza kwa DJs Juma Ramadhani,Msindi wa Pili katika kategori ya ma-MCs
Nchana Antony na Mshindi wa MCs Joash Magadula a.k.a MC Magadash.(Picha ya
Executive Solutions)
Picha na bin zubeiry |