SEHEMU YA MGUU AMBAO PIA ULIKATWA NA MAPANGA |
Saturday, December 29, 2012
MAUAJI YA BODABODA
Thursday, December 20, 2012
BODABODA MUSOMA ACHINJWA
Thursday, December 13, 2012
mtu adondoka kwenye ndege london
Picha ya mtu aliyeanguka kutoka kwenye ndege wakati inatua jijini London.
POLISI wa Jiji la London, Uingereza, bado wanahangaika kujua uraia wa
mtu mmoja wanayeamini alitoka Afrika na ambaye alianguka na kukutwa
amekufa baada ya ndege moja kufungua milango ya magurudumu yake wakati
inataka kutua uwanja wa Heathrow mwezi Septemba mwaka huu.Polisi hao wana picha ya mtu huyo iliyotayarishwa kwa kompyuta.
Vilevile, wachunguzi wanaamini mtu huyo anaweza kuwa alikufa muda mfupi tu baada ya ndege kuondoka ardhini ilikotokea, kutokana na kukosa hewa na kupigwa na ubaridi mkali wakati ndege ikiwa juu, hususani kwa vile alikuwa amejichimbia sehemu yanakoingia magurudumu ya ndege.
Tuesday, December 11, 2012
MAAJABU YA AFRICA MASHARIKI
Monday, December 10, 2012
WAZEE NA WASAAFU WA WILAYA NA MKOA WA MARA WANENA
Baada ya mbunge wa musoma mjini kupitia chama cha maendeleo CHADEM MH
VICENT NYERERE , jana kutoa tamko kuhusu matukio mbalimbali yanayodaiwa kutokea mkoni hapa Wataafu Viongozi wa vyama vya Siasa na Serikali, Wachungaji na Mashehe Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara wamekanusha vikali taarifa zilizochapishwa kwenye baadhi ya magazeti na Televisheni nchini kuwa ndani ya wilaya hiyo watu 17 wakiwemo wanawake 5 wamechinjwa kati ya Oktoba hadi Desemba mwaka huu.
Wazee hao pia waliiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo kumkamata mwandishi wa habari hizo ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria kutoa ushahidi wa watu waliochinjwa kisha kumfikisha mahakamani kujibu mashitaka ya kuandika habari za uzushi na uchochezi na kuwatia hofu wananchi.
Wakizungumza na Mkuu wa Wilaya hiyo Jackson Msome na kamati yake ulinzi na usalama kwenye kikao cha dharura kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha Waganga katika Manispaa hiyo wazee hao kwa kauli moja walimuhakikishi Mkuu wa wilaya hiyo kuwa habari hizo ni za uzushi zenye kuwatia hofu wananchi.
“Ukisoma kwenye haya magazeti utagundua habari hii imekaa kisiasa kwani hata Mbunge wa Chadema Vicent Nyerere anadiriki kusema kuwa anamtaka IGP said Mwema akomeshe mauaji hayo pia kamati ya ulinzi na usalama imekalia siasa huu ni uzushi na tunapinga kama kuna ukweli tunaomba otoe ushahidi kwa kuonyesha maiti zilizochinjwa,”alisema Mzee Seleman Kerenge.
Alisema kuwa vyombo hivyo vya habari vinalengo vya kuvuruga hali halisi ya amani na usalama ndani ya mji wa Musoma na kudai kuwa hakuna mtu yeyote aliwahi kuchinjwa ndani ya Manispaa hiyo.
Mzee Abdu Husein wa Makoko alisema kuwa wazazi wengi nchini hawapendi kutoa matatizo ya watoto wao hata kama wanashiriki katika vitendo viovu ambapo wanazua matatizo makubwa kwenye jamii.
“Tuna mapungufu makubwa sisi kama wazazi hata kama unajua matatizo ya vijana wako hutaki kusema ukweli, wazazi wengi hata vikao na vijana wao hawafanyi, tuna mamlaka lakini hatuyatumii,”alisema Husein kwa hasira kubwa.
Akitoa taarifa mbele ya wazee na mkuu wa wilaya Kaimu kamanda wa Polisi katika wilaya hiyo Lucas Hupa alisema kuwa matukio ambayo yalitokea katika kipindi cha mwezi Oktoba na Novemba ni matatu.
Alisema kuwa tukio la kwanza lilitokea Oktoba 19, Enock ambaye
alikuwa mlinzi alifariki dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Mara baada ya kukatwa kwa mapanga na watu wanaodaiwa kuwa majambazi.
Tukio la pili lilitokea Oktoba 28, mwaka huu ambapo Msichana Lilian Bonifance (12) aliuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa na tukio la mwisho lilitokea Novemba 21 ambapo mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya Salama aliuawa na watu wanaodai kuwa majambazi.
Hupa alisema kuwa tayari jeshi hilo linawashikilia watu 16 na
watuhumiwa nane walisomewa mashitaka ya mauaji na kupelekwa magereza.
Naye Mkuu wa Wilaya Msome alisema kuwa kuna matukio yapo ndani ya wilaya hiyo lakini sio kama inavyozungumzwa kwa sasa ambapo ni hali ya kuwatisha wananchi wa Manispaa hiyo.
“Waandishi wa habari ni ndugu zetu wote tunafanya kazi kwa kuwatumikia wananchi tuache kuandika habari za uzushi na uchochezi ambazo zinatia hofu wananchi wetu,”alisema Msome.
Msome alisema kuwa Waandishi wa habari hawajaitendea haki Manispaa hiyo kutokana na habari hiyo ambayo alisema kuwa ni ya uzushi na kuwaomba kuandika habari sahihi ambazo hazipotoshi umma.
“Madhumuni ya vyombo vya habari na kazi ya mwandishi wa habari ni kufundisha, kuburudisha na kuelimisha sio kupotosha na kuchochea hayo sio maaili ya uandishi wa habari,”alisema.
Baada ya ukanushaji wa mauaji hayo Msome amewaomba wazee, Viongozi naViongozi wa dini kushirikiana na kuanzisha ulinzi shirikishi ili kuepukana na uzushi kama huo uliotokea ambapo ataanza na mafunzo juu ya ulinzi huo ambao yataanza Desemba 13 mwaka huu kwa kata nne za Iringo, Mkendo, Kitaji na na zingine zitafuata.
Taarifa ambazo hivi karibuni zilitolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mara kupitia kwa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa huo, Japhet Lusingu kuwa ni matukio mawili ya watu kuchinjwa ndiyo yaliyoripotiwa na yalitokea katika Wilaya ya Butiama na sio watu 17 kama ilivyotangazwa.
Tukio la kwanza ni mwanawake aliyetambulika kwa jina la Blandina Peru (28) mkazi wa kijiji cha Mahare, kata ya Etaro aliuwawa Desemba 2 mwaka huu kwa kukatwa koromeo na kubakwa na wauaji kabla ya kumuua wakati akiwa porini akikata kuni na watuhumiwa wa tukio hilo bado hawajakamatwa.
Tukio la pili lilitokea Kijiji cha Kabegi, Kata ya Nyakatende, Wilaya
hiyo hiyo ambapo Sabina Mkireri (44) mkazi wa kijiji cha kiemba
aliwawa kwa kuchinjwa shingo na kichwa chake kuchukuliwa na watu wasiojulikana katika kijiji cha kabegi na watu sita wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.
MBUNGE WA MUSOMA MJINI
MH MBUNGE WA MUSOMA MJINI KUPITIA CHADEMA VICENTI KIBOKO NYERERE
wananchi wengi wa jimbo ilo walijitokeza kwa wingi katika viwanja vya shule ya msingi mukondo musoma mjini MH VICENT NYERERE aliambatana na aliyekuwa mbunge wa ARUSHA mjini MH GODBLES LEMA .
Katika Mkutano huo ambao ulimalizika kwa Wananchi kuwasindikiza kwa msururu Mkubwa kutoka katika viwanja hivyo hadi katika makao makuu ya Chama hicho Wilaya ya Musoma Mjini kwa nyakati tofauti wanasiasa hao walitumia jukwaa kulaani matukio ambayo yamekuwa yakitokea yakiwemo ya mauaji.
Awali Mbunge wa jimbo la Musoma Mjini Visenti Nyerere alitumia jukwaa hilo kusikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya kushindwa kufika katika mkutano huo licha ya kualikwa kutoa ufafanuzi kwa Wananchi kutokana na matukio mbalimbali ya mauaji ambayo yamekuwa yakitangazwa na yeye kukanusha.
"Akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya tumemualika kuja kutoa ufafanuzi kwa Wananchi juu ya yale yanayoelezwa lakini ameshindwa kufika na matokeo yake anatutumia ujumbe kwa njia ya simu akisema yupo kwenye sherehe za miaka 51 ya Uhuru huu si uungwana na tunasema yeye ameshindwa kuja tukisikia mtu mwingine amekufa tutaandamana kushinikiza aondoshwe katika Wilaya hii.
"Sisi hatutaki kujua idadi ya watu waliofikwa na matukio ya kuchinjwa hata kama amechinjwa mtu mmoja suala ni kutokea kwa tukio hilo hivyo akiwa kama mkuu wa Amani katika Wilaya alipaswa kuitika wito wa Mkutano huu na kuwaondoa hofu Wananchi kutokana na yale yaliyoelezwa",alisema Nyerere
Alisema suala hilo halikuwafurahisha lakini pia Mbunge huyo akamtaka Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mara Absalom Mwakyoma kukatisha likizo yake ili kuja kutoa ushirikiano katika kukabiliana na matatizo yaliyojitokeza katika siku za hivi karibuni hali iliyopelekea Wananchi kuwa na hofu na kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo.
Akizungumzia suala la Maendeleo Nyerere alisema akiwa kama Mbunge kwa kushirikiana na Balaza la Madiwa linaloongozwa na Chadema watahakikisha yale yote waliyoyaleza katika kipindi cha kampeni yanatekelezwa nakuomba Wananchi waendelee kutoa ushirikiano katika kufanikisha.
"Wananchi wenyewe mnaona kwa kipindi cha muda mfupi barabara nyingi ambazo zilikuwa hazipitiki lakini leo zinapitika na kufika katika maeneo mbali yaliyokuwa korofi na haya ni maeneo machache katika miundombinu lakini pia hata katika miradi mingine ikiwemo ya maji utekelezaji wake unafanyika.
"Tumepata Bilioni 13 kutoka benki ya Dunia katika miradi ya barabara tunawahahakishia Wananchi fedha hizi zitafanya kazi kama zilivyoelekeza na zipo barabara ambazo zitakuwa na kiwango cha lami na nyingine za kiwango cha changarawe na tunataka kufikia mwaka 2013 mwishoni kila barabara iweze kupitika.
Kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Godbles Lema yeye aliwataka Wananchi kutokuwa moyo wa uoga katika kudai haki zao za msingi na kutoa ushirikiano na kushirikiana na viongozi wa Chadema katika kutafuta mabadiliko na badala yake kukaa pembeni na kuanza kulalamikia kila wakati.
"Nimewapenda vijana wa Musoma nyie ni Jasiri kama walivyo vijana wa Arusha ambao kila kukicha wanatamani mabadiliko lakini naamini ipo siku itafika na kile tunachokitaka kitafanikiwa lakini nawaomba ondoeni moyo wa uoga jengeni ujasiri na shirikianeni na viongozi wenu katika kutaka kujikomboa.
"Haina maana kila wakati kukaa pembeni na kuanza kulalamika maana mabadiliko hayaji kwa kulalamika tujitoe na tushirikiane katika kufanikisha kile ambacho tumekuwa tukikitaka ili kila mmoja aweze kunufaika na rasilimali zilizopo katika Nchi hii ambazo zimekuwa zikiwanufaisha watu wachache",alisema Lema
Lema alisema kila mmoja kwa nafasi yake anao wajibu wa kuhakikisha analeta mabadiliko na sio kazi ya kuwaachia viongozi pekee yao katika kuyatafuta huku wengine wakikaa pembeni na kuanza kulalamika kwani malalamiko yao yatakuwa hayana maana katika kufikia malengo ambayo yanakusudiwa.
Friday, December 7, 2012
MARA PRESS CLUB TARIME
TAALIFA YA JESHI LA POLISI MARA
JAPHET LUSINGU-KAIMU KAMANDA WA POLISI MARA, MUSOMA
Jeshi la
Polisi Mkoani Mara limekanusha uvumi wa kutishia wananchi toka kwa baadhi ya
watu wenye nia mbaya kuwa ndani ya mwezi mmoja watu 15 wameuwawa kwa kuchinjwa.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mara, Musoma Japhet
Lusingu imedai kwamba hivi karibuni kumekua na uvumi kuwa katika Mkoa wa Mara
wananchi wamekuwa wakichinjwa na tayari watu 15 wameuwawa kwa kuchinjwa kitu
ambacho ni uongo.
Kaimu
kamanda huyo amesema kutokana na uvumi huo wamekua wakipokea simu toka kwa
wananchi na viongozi ndani ya manspaa ya Musoma katika kata ya nyakato kwamba
kuna kuna mwanafunzi ameonekana ameuwawa kwa kukatwa kichwa katika makaburi ya
Musoma bus na jeshi la polisi likifuatilia wanakuta ni taarifa za uongo na za
kuwatisha wananchi.
Amesema kuna
matukio mawili wanawake kuuwawa vichakani katika vijiji vya Mmahare kata ya
Etaro ambapo Blandina Peru (28) aliuwawa 2.12.2012 kwa kukatwa koromeo na
kubakwa na wauaji kabla ya kumuua wakati akiwa porini akikata kuni na watuhumiwa
wa tukio hilo bado hawajakamatwa.
Tukio la
pili lilitokea Kabegi kata ya Nyakatende wilayani butiama ambapo Sabina Mkireri
(44) mkazi wa kijiji cha kiemba aliwawa kwa kuchinjwa shingo na kichwa chake
kuchukuliwa na watu wasiojulikana katika kijiji cha kabegi na watu sita wanashikiliwa
na jeshi la polisi kwa mahojiano.
Kutokana na
uvumi huo amewatoa hofu wananchi juu ya
mauaji hayo na kuwatahadharisha akina mama hasa maeneo ya vijijini wanapokua
katika shughuli zao za kilimo na utafutaji wa kuni wawe waangalifu na watoe
taarifa mapema wanaposhuku jambo lolote lisilo lakawaida.
Ameongeza
kuwa kwa sasa wanaendelea na msako maeneo mbalimbali ya manispaa ya Musoma na
wilaya ya butiama ambapo kuna watu watano wanashikiliwa na jeshi hilo kwa kwa
makosa yakupatikana na pombe haramu ya gongo na wengine wanashikiliwa kwa
kupatikana na bangi na wote watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi
kukamilika.
Katika hatua
nyingine amewataka wananchi wenye taarifa za uhalifu na wahalifu wasisite
kulijulisha jeshi la polisi kupitia kwa viongozi wa maeneo yao.
Thursday, November 29, 2012
WATU WAWILI WAFARIKI MARA
mtummoja jisia ya kiume asiyefahamika kwa jina aliuwa na wananchi wenyehasila kali baada ya kukutwa akiiba mabati toka kwenye jengo la mtu aitwaye JUMANNE KAGOSI,mnamo tarehe 29/11/2012 majira ya saa 04.00 usiku katika kijiji cha kwangwa kata ya kigera manispaa ya musoma mkoa wa mara.
akizungumza na waadishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa mara S.A.C.P ABSALOM .A.MWAKYOMA amesema kuwa upelelezi unaendelea kubaini waliohusika na tukio hilo,na kuwakamata ili hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani zichukuliwe.
pia kamanda wa polisi mkoa wa mara anatoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
na wilayani serengeti mugumu katika kijiji cha soguti kata ya ikorongo tarafa ya Ngoreme bw MWITA NYAITATI CHACHA umri wa 35,mkulima wa suguti aliuwawa kwa kukatwakatwa na mapanga kichwani
mkono wa kushoto na mkono na mguu wa kulia na wananchi waliojichukulia sheria mkononi.
hayo yamesemwa leo na kamanda wa polisi mkoa wa mara ABSALOM .A.MWAKYOMA ofisini kwake
amesema kuwa chanzo cha tukio ni baada ya marehemu kukamatwa na ng"ombe ya wizi mali ya PHILIMON MUNDU wa kijiji cha musati uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
akizungumza na waadishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa mara S.A.C.P ABSALOM .A.MWAKYOMA amesema kuwa upelelezi unaendelea kubaini waliohusika na tukio hilo,na kuwakamata ili hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani zichukuliwe.
pia kamanda wa polisi mkoa wa mara anatoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
na wilayani serengeti mugumu katika kijiji cha soguti kata ya ikorongo tarafa ya Ngoreme bw MWITA NYAITATI CHACHA umri wa 35,mkulima wa suguti aliuwawa kwa kukatwakatwa na mapanga kichwani
mkono wa kushoto na mkono na mguu wa kulia na wananchi waliojichukulia sheria mkononi.
hayo yamesemwa leo na kamanda wa polisi mkoa wa mara ABSALOM .A.MWAKYOMA ofisini kwake
amesema kuwa chanzo cha tukio ni baada ya marehemu kukamatwa na ng"ombe ya wizi mali ya PHILIMON MUNDU wa kijiji cha musati uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Thursday, November 22, 2012
pikipiki za kubebea wa gonjwa.zageuzwa makumbusho musoma (v)
Wednesday, November 21, 2012
pendo malima asimulia kichapo alichopata kutoka kwa mumewe
pendo akiwa na mama yake monica malima wodini |
Friday, November 16, 2012
TUME YA KATIBA YAANZA KAZI MKOA WA MARA
Emmanuel bwimbo wa mrpc na beldina nyakeke |
maxmilia ngessi wa rfa, fazeli janja wa kulikoni na veronica wa majira,frolence wa nipashe na george marato wa itv |
ghati,bigambo jeje wa( voa) na pascal buyaga wakimsikiliza rc wa mkoa |
Wednesday, November 14, 2012
WAKENYA WAZINDUA HUDUMA YA TRENI JIJI NAIROBI
Tuesday, November 13, 2012
Thursday, November 8, 2012
HALIMA MDEE NA HOJA BINAFSI BUNGENI
siku ya walipa kodi mkoani mara
katibu wa chama cha wanahabri berdina akipokea kombe baada ya timu ya wahandishi wa habari kuibuka kidedea kwa kuifunga timu ya TRA mabao 2-1 |
mwanafunzi wa mwenbeni secondri akipokea zawadi baada ya kuwa mshidi wa maswali mbalimbali kuhusu TRA. |
kamanda g.marato akipokea zawadi kwa niaba ya ITV. |
armasi kutoka TBC 1 nayeakipokea zawadi. |
meneja wa TRA mara akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi. |
Thursday, October 25, 2012
MAGUFULI AKUBALI OMBI
![]() |
makabidhiziano yafanyika mbele ya waziri mwenye dhamana. |
![]() |
mhandisi patrick mfukule kushoto na mtendaji mkuu kutoka kampuni ya ujenzi ya china raylway 15 Bureau group corporation (CR15G) Zhang tonggang (kulia) wakiweka saini. |
Thursday, October 18, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)