Saturday, December 29, 2012

MAUAJI YA BODABODA

MADEREVA WA PIKIPIKI WAKIPITA KATIKA BARABARA YA MKENDO KWENDA KUMSHUHUDIA MWENZAO HOSPITALI YA MKOA WA MARA

SEHEMU YA MGUU AMBAO PIA ULIKATWA NA MAPANGA  

BODABODA WAKIWA NJE YA HOSPITALI YA MKOA WA MARA

MWENZAO ACHINJWA


Mbunge atangaza vita na Nyani waharibifu

          -Mwananchi atakayeua nyani na kumpelekea mkia kulipwa elfu kumi



Mbunge wa Jimbo la Kibara Kangi Lugora (CCM) ametangaza vita na Nyani ambao amedai wamekuwa wakiharibu mazao ya Wananchi mashambani na wengine kuwadhuru watu katika maeneo yao ya makazi na kupelekea kukwamisha shughuli za kiuchumi zinazofanywa na Wananchi katika Jimbo hilo.

Akizungumza na BLOGU HII Mjini Bunda Kangi alisema tayari walishatoa taarifa Serikalini kupitia Wizara ya Mali Asili na Utalii kuhusiana na uharibifu unaofanywa na Nyani hao lakini wamekuwa kimya bila kuchukua hatua zinazostahili hivyo amaeamua kuwahamasisha Wananchi katika Jimbo lake kuhakikisha wanawaangaamiza Nyani wote katika maeneo yao.

Alisema nyani hao wamekuwa wakifanya uharibifu mkubwa ambao wameshindwa kuuvulia wakati walishatoa taarifa katika sehemu zinazohusika na kukaliwa kimya hivyo wameamua kwa nguvu zao kuhakikisha wanapambana na nyani hao na kuwaondoa kabisa katika maeneo yao.

Mbunge huyo alisema amewaajili watu watano ambao wanatumia siraha za bunduki na kijadi kuhakikisha popote wanakutana na nyani  kuwaua ili wasiendelee kuharibu mazao ya Wananchi na kuwadhuru binadamu kwa kuwa Serikali imeshindwa kulichukulia hatua suala hilo.

Alisema licha ya kuwaajili watu hao pia amewatangazia ajira Wananchi wa Jimbo hilo kwa yeyote atakaye ua nyani na kisha kumpelekea mkia atapewa shilingi elfu kumi papo hapo kwa kuwa amewaweka mawakala ambao wanatumia stakabadhi ambazo zimeandaliwa kwa kazi hiyo ya kuwalipa Wananchi.

"Hatuwezi kuendelea kukubaliana na hali hii ya kuharibiwa mazao yetu huku Serikali imekaa kimya tutawaua nyani wote kwa kuwa hawana faida kwetu na nimeshaandaa fedha za kutosha ambazo kila Mwananchi atakayefanya kazi hiyo atapata malipo yake,"alisema Kangi.

Alisema nyani hao wamekithiri sana katika milima ya Lagata,Ilamba na Kitengere ambapo amedai huko kote amewaweka mawakala ambao watahakikisha kila Mwananchi atakayepeleka mkia wa nyani anapata malipo yake papo hapo pasipo usumbufu.

"Kwanza nyani hawa sio utalii kwetu na hakuna mtu yeyote anayekuja hapa kufanya utalii wa kuangalia nyani na kama Serikali ingeona wanafaa kwa utalii wangesikiliza vilio vya Wananchi kutokana na adha wanayoipata ya kuharibiwa mazao yao na kuwadhuru Wananchi,"alisema Mbunge huyo. 

Mbunge Kangi aliongeza kuwa licha ya uharibifu wa nyani hao lakini pia kumekuwepo na matukio ya Wananchi kudhuliwa na Mamba pamoja na Viboko katika Ziwa Victoria ambapo pia wameanzisha vita ya kuhakikisha wanawawinda mamba pamoja na viboko na kuwaua.

Alisema hadi sasa watu wanne wameuwawa na mamba pamoja na viboko huku Serikali ikikaa kimya hivyo wao wameamua kuanzisha mapambano ambayo yatawaangamiza mamba na vibiko wote ambao wamekuwa wakiwadhuru Wananchi. 

.....................................................................................................................................

    Profesa Muhongo aijibu CUF kuhusu mgawo wa umeme



WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesisitiza kuwa hakuna hoja ya mgawo wa umeme kwa sasa hapa Nchini kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kujipanga kutafuta vyanzo vingine vya uzalisha mbadala wa umeme kuliko kutegemea maji ili ifikapo Mwaka 2013 Tanzania iweze kupata umeme wa uhakika.

Kauli hiyo ameitoa Mjini hapa katika kikao kilichowashilikisha Vijana wa Manispaa ya Musoma kutaka kujua ni changamoto gani zinazopelekea Mji huo kukosa Maendeleo na kuzungummzia jinsi Shirika hilo linavyoendeleaa kufanya mabadiliko katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi na kupata umeme wa uhakika.

Alisema anapingana na maazimio yaliyotolewa na Chama cha Wananchi (CUF) katika Baraza lake Uongozi lilofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam na kueleza kuwa upo mgawo usio rasmi wa umeme ambao unapelekea kero kwa Wananchi na kukwamisha shughuli za kimaendeleo ambazo zinahitaji nishati ya umeme.

Profesa Muhongo alisema suala la kukatika kwa umeme kwa dakika mbili ama tatu sio mgawo kama inavyoelezwa na Chama hicho bali ni kutokana na miundombinu ambayo imechakaa ambapo kwa sasa Tanesco imeelekeza katika kufanya jitihada za kuibadilisha ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo.

''Sote tunafahamu miundombinu ya Shirika hili mingi imechakaa na inahitaji mabadiliko ambayo kwa sasa kwa asilimia kubwa inafanyiwa kazi hivyo inapelekea kuwepo na kero ya kukatika kwa umeme kwa muda furani lakini sio kila siku na huo sio mgawo wa umeme jamani tuache propaganda za kisiasa katika masuala mengine ya maslahi ya Taifa,"alisema Muhongo.

Alisema yeye akiwa kama Waziri mwenye dhamana ya umeme atamueleza Waziri Mkuu ama Rais iwapo kutakuwa na mgawo wa umeme lakini sio watu kusimama na kusema kuna mgawo kitu ambacho amekiita ni uzushi ambao unatumiwa na wanasiasa katika propoganda zao ambazo hazina tija kwa Taifa.

Alidai Tanesco inajipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana na tayari imeanza programu ya kusambaza umeme Nchi nzima katika Vijiji na Wilaya na kusema kazi hiyo inahitaji kupana ushirikiano katika kuifanukisha na kuomba kupata maoni kwa kila Mwananchi namna ambavyo anataka shirika hilo lifanye katika kuleta ufanisi tofauti na kipindi cha nyuma

Aidha Profesa Muhongo alisema zipo changamoto nyingine ambazo zinafanywa na watu wasio wazalendo kwa kuiba mafuta ya Transifoma pamoja na waya za umeme hali inayopelekea kujitokeza kwa matatizo ya kukatika kwa umeme ili kupisha mafundi kuweza kurekebisha na kurudisha umeme na kuwaomba Wananchi kuweza kutoa taarifa pale wanapoona mtu anataka kuhujumu shirika hilo.

Akizungumzia masuala ya kimaendeleo katika Mji wa Musoma,Waziri Muhongo aliwataka vijana wa Mji huo kuacha ubinafsi na kushirikiana katika kujitafutia Maendeleo na kubadilisha muonekano wa Mji huo na kusisitiza kujiepusha na kukalia siasa muda wote bali wajishughulishe na shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo.
 

.................................................................................................................................

                          Amuuwa mtoto kwa kumchapa fimbo


MKAZI mmoja wa kata ya Nyasho katika Manispaa ya Musoma aliyefahamika kwa jina la Yohana Msafiri (38) amemuuwa mtoto wake Veronica Yohana kwa kumchapa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake Desemba 23 na kupelekea kifo chake akiwa njiani kupelekwa hospitali baada ya kuzidiwa na maumivu.

Katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari,Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mara Absalom Mwakyoma  alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 usiku katika maeneo hayo ya Nyakato ambapo chanzo cha kuchapwa viboko kwa mtoto huyo na matatizo ya kifamilia.

Alisema mzaza wa Mtoto huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na tukio hilo ambapo amedai mara baada ya kukamilika kwa upelelezi mzazi huyo atafikishwa Mahakamani kuweza kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kutokana na tukio hilo Kamanda Mwakyoma amewataka wazazi kuangalia adhabu mbadala ambazo wanaweza kuwapa watoto pale wanapokuwa wanafanya makosa katika kuwafunza na sio kuwa na hasira ambayo inaweza kupelekea madhara mengine makubwa zaidi.

"Wazazi lazima waangalie adhabu mbadala ambazo zinapaswa kupewa watoto pale wanapofanya makosa maana kwanza ifahamike hawa ni watoto na yaale wanayoyafanya ni kutopkana na utoto wao hivyo iwepo busara katika kutaka kutoa adhabu kwa watoto wetu,"alisema Kamanda Mwakyoma.

Katika tukio lingine Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi Mkoani Mara alisema mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Gogogo anayekadiliwa kuwa na umri kati ya m,ika 40 na 45 mkazi wa Bunda aliyekuwa akiishi kata ya Nyakato Mshikamano katika Manispaa ya Musoma aliuwawa kwa kushambuliwa na kuchomwa moto kwa kudaiwa anahusika katika matukio ya ujambazi.

Kamanda Mwakyoma alisema Wananchi wanapomuhisi mtu anashiliki katika matukio ya uhalifu ni vyema kutoa taarifa Polisi na si kujichukulia sheria mkononi kwani hata kama mtuhumiwa anashiliki anapokamatwa anaweza kutoa taarifa ambazo zinaweza kuwapata watu wengine ambao anashiliki nao katika matukio hayo.

Alisema kujichukulia sheria mkononi ni kosa kwa mujibu wa sheria na atakaye kamatwa kutokana na kosa la kujichulia sheria mkononi atafikishwa Mahakamani kutokana na kosa hilo na kutoa tahadhari kwa Wananchi kuacha tabia hiyo kwani haifai na sheria hairuhusu kujichukulia sheria mkononi.

....................................................................................................................................






     

No comments:

Post a Comment