mtummoja jisia ya kiume asiyefahamika kwa jina aliuwa na wananchi wenyehasila kali baada ya kukutwa akiiba mabati toka kwenye jengo la mtu aitwaye JUMANNE KAGOSI,mnamo tarehe 29/11/2012 majira ya saa 04.00 usiku katika kijiji cha kwangwa kata ya kigera manispaa ya musoma mkoa wa mara.
akizungumza na waadishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa mara S.A.C.P ABSALOM .A.MWAKYOMA amesema kuwa upelelezi unaendelea kubaini waliohusika na tukio hilo,na kuwakamata ili hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani zichukuliwe.
pia kamanda wa polisi mkoa wa mara anatoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
na wilayani serengeti mugumu katika kijiji cha soguti kata ya ikorongo tarafa ya Ngoreme bw MWITA NYAITATI CHACHA umri wa 35,mkulima wa suguti aliuwawa kwa kukatwakatwa na mapanga kichwani
mkono wa kushoto na mkono na mguu wa kulia na wananchi waliojichukulia sheria mkononi.
hayo yamesemwa leo na kamanda wa polisi mkoa wa mara ABSALOM .A.MWAKYOMA ofisini kwake
amesema kuwa chanzo cha tukio ni baada ya marehemu kukamatwa na ng"ombe ya wizi mali ya PHILIMON MUNDU wa kijiji cha musati uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
No comments:
Post a Comment