Monday, January 21, 2013

MATEKA WALIOUAWA ALGELIA WAONGEZEKA

 


                         Wanajeshi wa Algeria wadhibiti uwanja wa Ndege mjini Ain Amenas
 

                             Kiongozi wa wapiganaji wa kiisilamu Algeria Mokhtar Belmokhtar

 Wanajeshi wanaendelea na upekuzi katika eneo kulipotokea utekaji nyara katika kiwanda cha mafuta cha Amenas. Ndani ya kiwanda hicho zaidi ya maiti ishirini zilizoteketea kiasi cha kutoweza kutambulika zilipatikana.
 Kufikia sasa idadi ya waliofariki katika kisa hicho imefikia 80.
Hata hivyo, bado haijabainika ni wangapi miongoni mwa waliopfariki walikuwa mateka
Taarifa zaidi zinarifu kuwa Maiti za mateka kutoka Japan, Norway, Uingereza, Marekani na Malaysia bado hazijatambuliwa huku maafisa wa usalama wakisema kuwa watekaji nyara watano tayari walithibitishwa kuuawa na wapiganaji.
Takriban mateka 48 wameaminika kuuawa katika siku nne za sokomoko kwenye kiwanda cha gesi nchini Algeria.
Wanamgambo 5 inaarifiwa walikamatwa hiyo Jumapili
Maafisa wa utawala awali walisema Jumamosi kuwa watekaji nyara 32 waliuawa.
Hata hivyo makomando waliweza kumaliza vurugu hilo siku ya Jumamosi. Maafifa walisema kuwa idadi kamili ya watu waliofariki itatolewa baadaye.
Jeshi lililazimika kufanya operesheni hiyo baada ya wanamgambo hao kuanza kuwaua mateka.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na rais wa Marekani, Barack Obama, wamelaumu magaidi kwa kusababisha vifo vya mateka.
Kiongozi wa wapiganaji wa kiisilamu Algeria Mokhtar Belmokhtar
Kingozi wa wapiganaji hao, Mokhtar Belmokhtar, alisema kuwa wako tayari kufanya mazungumao na serikali ya Algeria lakini sharti wakome kushambulia wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali.
Na Jumapili, waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, alitaja kitendo cha wanamgambo hao kama kitendo cha vita.



               Ufaransa wadhibiti Diablay




                                                 Harakati za jeshi la kigeni nchini Mali
  
Wanajeshi wa Ufaransa na wa Mali, wameingia katikati mwa mji wa Diabaly, bila ya makabiliano yoyote na wapiganaji wa kiisilamu.
Msururu wa magari 30 ya kijeshi yaliyokuwa yamewabba wanajeshi 200 wa Mali na Ufaransa, yalionekana yakielekea mjini humo.
Wapiganaji walitoroka Ijumaa baada ya mji huo kushambuliwa kwa ndege za kijeshi
Ufaransa ilianza operesheni yake ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali wiki moja iliyopita ili kujaribu kuwaondoa wapiganaji wanaodhibiti Kaskazini mwa Mali.
Jeshi la Ufaransa linanuia kuweza kudhibiti eneo hilo kikamilifu kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu. Hii ni kwa mujibu wa waziri wa ulinzi wa Ufaransa,Jean-Yves Le Drian.
"hatutaondoka bila ya kuwafurusha kabisa wapiganaji hao, '' waziri aliambia vyombo vya habari.
Ufaransa imetuma takriban wanajeshi 2,000 kusaidia Mali kupambana na wapiganaji hao wa kiisilamu.


              Muasi wa Nigeria hatiani A. Kusini





                                          Henry Okah kiongozi wa kundi la waasi la Mend
Mahakama nchini Afrika Kusini imempata na hatia ya vitendo vya kigaidi kiongozi wa waasi wa Nigeria Henry Okah.
Okah anasemekana kupanga mashambulizi ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari na kuwaua watu 12.
Okah alipatikana na hatia ya makosa 13 kuhusiana na vitendo vya kigaidi.
Alikamatwa mjini Johannesburg siku moja baada ya mabomu mawili kulipuka wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Nigeria.
Alikanusha makosa hayo ingawa kundi analoongoza la Mend, lilikiri kutekeleza mashambulizi hayo.
Jaji wa mahakama kuu mjini Johannesburg, Neels Claassen, alimpata na hatia Okah ya makosa ya kupanga njama ya mashambulizi pamoja na kufanya vitendo vya kigaidi ikiwemo kulipua mabomu.
"ushahidi ambao ulitolewa na washirika wake haukupingana,'' alisema jaji Claassen
Okah alikamatwa kwa kosa la kumiliki bunduki kinyume na sheria nchini Angola mwaka 2007 na kisha kuhamishwa hadi nchini Nigeria ingawa hakuwahi kuhukumiwa.
Aliachiliwa baada ya miaka miwili chini ya msamaha uliotolewa kwa wapiganaji walio katika maeneo ya mafuta na ndipo aliporejea Afrika Kusini ambako aliishi hadi mwaka 2003.



Thursday, January 17, 2013

NIGERIA YAWASILI MALI



Itakuwa afueni kwa jeshi la Ufaransa pindi wanajeshi wa Nigeria watakapoanza kuwasili


Daraja ya Mali kuelekea Nigeria na hapa kuna kizuizi cha polisi

Takriban wanajeshi 200 wa Nigeria wanatarajiwa kuwasili nchini Mali kusaidia katika harakati dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu Kaskazini mwa nchi.
Ni kikosi cha kwanza cha jeshi kutoka Magharibi mwa Afrika kujiunga na wanajeshi wa Ufaransa walioanza kupambana na wapiganaji wa kiisilamu tangu Ijumaa iliyopita.
Jumla ya wanajeshi 3,300 wa kikanda watapelekwa nchini Mali chini ya azimio la Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa. Chad imesema itapeleka wanajeshi 2,000.
Wakati huohuo, wanajeshi wa Mali na Ufaransa, wameanza operesheni yao ya ardhini dhidi ya wapiganaji hao wa kiisilamu.
Duru zinasema kuwa makabiliano yalizuka kati ya waasi na wanajeshi mjini Diabaly, umbali wa kilomita 350 kaskazini mwa mji mkuu Bamako siku ya Jumatano.

Wapiganaji wa kiisilamu waliingia mji wa Diabaly siku ya Jumatatu na kutwaa mji huo kutoka kwa waasi. Ndege za kivita za Ufaransa tayari zimeshambulia ngome moja ya waasi hao.
Takriban wanajeshi 190 wa Nigeria wanatarajiwa kwenda kwa ndege nchini Mali kutoka Kaduna baadaye leo.

Daraja ya Mali kuelekea Nigeria na hapa kuna kizuizi cha polisi
Nigeria itaongoza kikosi cha nchi za Afrika Magharibi. Imeahidi kupeleka wanajeshi miatisa pamoja na ndege za kivita.
Chad pia imethibitisha kutuma wanajeshi 2,000 watakaojiunga na harakati dhidi ya wanajeshi nchini Mali.
Benin, Ghana, Niger, Senegal, Burkina Faso na Togo pia zimeahidi kutuma vikosi.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande alisema kuwa lengo na nia ya Ufaransa ni kuhakikisha uthabiti wa Mali.
Nchi hiyo imepeleka wanajeshi, 800 kupambana na waasi ardhini na duru za ulinzi zinasema kuwa idadi ya wanajeshi hao inatarajiwa kuongezeka hadi 2,500.
Hata hivyo, Ufaransa imekuwa ikishinikiza kutumwa kwa kikosi cha kanda ya Afrika Magharibi.

Kuwasili ka wanajeshi wa kwanza wa Nigeria itakuwa afueni kwa wale wa Ufaransa ambao hawajapata msaada wa kutosha kutoka kwa jeshi la Mali ambalo halina nguvu sana.

Wednesday, January 16, 2013

MAAZIMIO YA MKUTANO WA KAZI WA DC JACKSON MSOME NA VIONGOZI WA KATA ZA MUSOMA YAANZA KUTOLEWA TAALIFA

MH JACKSON MSOME  DC WA WILAYA YA MUSOMA MJINI AKIWEKA SAINI KATIKA KITABU CHA WAGENI BAADA YA KUFIKA KATIKA MKUTANO HUO KATIKA KATA YA KITAJI C MUSOMA MJINI LEO JIONI.

WAKWANZA KULIA NI MSHAULI WA MGAMBO NA WAPILI NI AFISA USALAMA WA WILAYA DSO PULE NA ALIYE SIMAMA NI MWENYEKITI WA KATA YA KITAJI C JUMANNE IDDI AKIMKALIBISHA MGENI RASMI.
TAALIFA FUPI ILISOMWA

MH DC AKIPOKEA TAALIFA FUPI YA UTEGELEZAJI WA MAAZIMIO YA MKUTANO WA KAZI WA MKUU WA WILAYA NA VIONGOZI WA KATA NA MITAA ULIOFANYIKA TAREHE 13/12/2012 CHUO CHA AFYA MUSOMA


NAE M/KITI WA KITAJI C JUMANNE IDDI ALIMKABIDHI MAJINA YA VIJANA WALIOTAJWA NA WAKAZI WA MITAA YA SHABBAN NA MAKONGOLRO KUWA WANAFANYA NA KUSHIRIKI KATIKA UKABAJI,WIZI,UBAKAJI NA VITENDO VIOVU NYAKATI ZA USIKU PAMOJA NA TAARIFA YA KAMATI YA ULINZI YA KATA YA KITAJI C MUSOMA MJINI.
MWENYEKITI WA KATA YA KITAJI AKIMKARIBISHA MH DCMSOME ALIPATA FULSA YA KUZUNGUMZA  NA WAKAZI WA KITAJI C NA KUWEKA MSISITIZO YA KWAMBA YALE MAAZIMIA 20 YALIYO WEKWA KATITA  MKUTANO WA KAZI 13/12/2012 KATIKA CHUO CHA AFYA SASA NI WAKATI WA UTEKELEZAJI KATIKA KILA MTAA,


 PIA AMESEMA KUWA KAMA WATABAINI UZEMBE WOWOTE WA KAMATI YA KATA YA ULINZI HATUA KALI KWA VIONGOZI WA KATA USIKA WATAWAJIBIKA PIA AMESEMA KUWA WALEVIJANA WOTE WALIYO TAJWA NA WANCHI NA HAWAKUFIKA KATIKA OFISI YA MWENYEKITI WA KATA KWAAJILI YA KUTOA MAELEZO WAFIKE MALAMOJA VINGINEVYO WAZAZI WATAWAJIBISHWA ,NA AMEOGEZA KUWA KAMATI YA WILAYA YA ULINZI NA USALAMA ITAPITA MITAA YOTE 57 KUPATA TAALIFA.

VIJANA 32 WAMECHAGULIWA NA KAMATI YA ULINZI YA KATA HIYO YA KITAJI C NAKUPEWA SEMINA YA JINSI YA KUFANYA DOLIA NYAKATI ZA USIKU SEMINA HIYO IMETOLEWA NA OCD WA JESHI LA POLISI WILAYA, AMEONYA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA KUUA MWALIFU PINDI WANAPO MKAMATA AMESIFU JINSI MAAZIO 20 NA MIKAKATI YA KATA HIYO KUWA YAMEFANYIKA VYEMA NA KUSEMA MPAKA SASA KILA KATA TEYALI IMEMALIZA MIKUTANO YAKE.

KATIKA SWALA LA KIPAUMBELE AMESEMA KUWA MATUKIO YA VIBAKA ,UDOKOZI NA MAUAJI KATIKA WILAYA NI LAZIMA KUPAMBANA NAYO NA MAKUNDI YA VIJANA BAADHI  YA WAZAZI WAMEALALISHA NA KUWAKUMBATIA VIBAKA HAO,PIA HATU YA KUTOA ONYO KWA WAZAZI NA WATOTO WAO NI LAZIMA ZICHUKULIWE MAPEMA NA YULE MZAZI ATAKAYE KWENDA POLISI KWAAJILI YA DHAMANA NA YEYE ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.AMEWAOMBA MAJILANI WA KAYA KUTOA TAALIFA KWA VIONGOZI WA KATA,WENYEVITI,VIONGOZI MBALIMBALI WA DINI N.K KUTOA TAALIFA YA MWALIFU WANAPO MGUNDUA.

AKIZUNGUMZIA SWALA LA VIJANA 32 WALIOCHAGULIWA AMESEMA KUA NI WACHACHE SANA NA KUSEMA KAMATI IKAEKUJADILI JINSI YAKUONGEZA VIJANA WENGINE.NA KUWAOMBA WAFANYA BIASHARA KUTOA USHIRIKIANO KWA VIJANA HAO ILI KULINDA MALIZAO AMESEMA KUWA BAA NA VILABU VYOTE VYA POMBE KUFUATA SHERIA YA LESENI ZAO .

MH DC JACKSON MSOME ALITOA FULSA YA MASWLI MATATU KATIKA MKUTANO HUO NA WATU  WALIULIZA MASWALI KWA DC MSOME.
SWALI  1 -IBRAHIM SHABBAN
               JE?  BAADHI YA WAZAZI WALIKANA BAADA YA KIJANA WAKE KUTAJWA  
                        JINA LAKE KUWA NI MUHUSIKA WA MATUKIO.

DC MSOME MAJIBU NI MZAZI ANATAKIWA KUWAJIBISHWA NA KUHOJIWA NA KAMATI YA WILAYA.

SWALI  2 - LUCAS MAKENDE
               JE? KIKOSI CHA VIJANA 32 NI WACHACHE SANA KWANINI WANANCHI
                      WASITOE MSAADA?
DC MSOME MAJIBU KWELI VIJANA 32 HAWATOSHI NAWAOMBA WANCHI WOTE AMBAO MTAKUWA NDANI YA NYUMBA KUAMKA MAPEMA MTAKAPO SIKIA FILIMBI YA VIJANA HAO ILA ANGALIZO MSICHUKUE SHERIA MKONONI ALISEMA DC MSOME.

SWALI LA 3 - HALIMA DAMAS
                    JE? MAENEO YA MAKABULI YA SHULE YA MSINGI MUSOMA NA KANISA                            LA MENONIGHT NI HATALI KWA VITENDO VYA UBAKAJI KWA
                           WANAFUNZI NA WAALIMU PIA NA MAEENEO YA OFISI YA CCM MKOA
                           NA UWANJA WA NDEGE PIA.
DC MSOME MAJIBU VIKOSI MAALUM TEYALI VIMEPANGWA MCHANA NA USIKU KUHAKIKISHA TUNAWABAINI WAALIFU HAO PIA AMEWAOMBA WANACHI KUTOA
TAALIFA KWA KIOGOZI YOYOTE WA KATA ALIYE KARIBU NA TUKIO ILITUWEZE KUJAMAPEMA ENEO LA TUKIO.

MWISHO ALIWAOMBA WAKAZI NA WANANCHI WOTE KUTOA TAALIFA ZA SILI KWA KIONGOZI YOYOTE ANAYE MUAMINI KUWA NI MSILI AU KUTUMA MESEJI KWAKE AU KWA OCD MOJA KWA MOJA.





MAUAJI YA KINYAMA TARIME

MAMA AUA MTOTO WAKE WA MIEZI 11 TARIME ,ANYOFOA BAADHI YA VIUNGO VYA KE



JESHI la polisi katika kanda maalumu ya Tarime na Rorya, linamshikilia mwanamke mmoja Prisca Mwita (22), mkazi wa mtaa wa Nyamisangura mjini Tarime, kwa tuhuma ya kunyofoa baadhi ya viungo vya mtoto wake mchanga na kusababisha kifo chake..
Kamanda wa polisi katika mkoa wa Kipolisi wa Tarime na Rorya, kamishina msaidizi  Justus Kamugisha, amesema kuwa  tukio hilo limetokea januari 11, mwaka huu, majira ya saa 2:00 asubuhi nyumbani kwa mwanamke huyo eneo la mjini Tarime.

Kamanda Kamugisha amesema kuwa mwanamke huyo anatuhumiwa kuua mtoto wake Happy Anthony mwenye umri wa miezi 11, baada ya kumkata sikio la kushoto, kumnyoa nywele za upande wa kushoto, kumnyoa nyusi za jicho la kushoto na kumchuna ngozi ya kichwa sehemu ya kushoto.
Amesema kuwa majirani waligundua unyama huo na kutoa tarifa kwa viongozi wa eneo hilo na kwamba mwanamke huyo  anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kuanzia leo .
tukio hilo limehusishwa na  imani za kishirikina, kwani ni la ajabu kwa mama mzazi kufanya unyama huo kwa mtoto wake.
...................................................................................................................................
 
Kamanda wa polisi mkoa wa mara absalom mwakyoma akitoa taarifa ya ajali mbele ya waandishi wa habari .
mabasi mawili jana jumapili yamegongana uso kwa uso na wilayani bunda mkoani mara na kusababisha  vifo vya watu sita papo hapo na mmoja kufikiaa hospitali teule ya wilaya ya bunda na kufikia idadi ya maiti saaba huku watu 47 wakijeruhiwa vibaya.

akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi Absalom Mwakyoma alisema kuwa ajali hiyo ilitokea  majira ya saa 11jioni  katika kijiji cha nyatwari Tarafa ya Serengenti wilayani bunda  karibu na hifadhi ya taifa ya Serengenti mpakani mwa mkoa wa mara na simiyu  na kuhusisha mabasi mawili  ya mwanza coach T756AWT aina ya scania marcopolo mali ya Halfan Ahmed wa mwanza likitoka  musoma kuelekea mwanza jina la dereva halikufahamika inaelekea alikimbia  dereva huyo na basi T535 AJR aina ya scania marcopolo bestline  lililokuwa likitokea mwanza kuelekea sirari wilayani tarime.

Mwakyoma alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa mabasi hayo na madereva kutokuwa makini  ambapo yalifika katika eneo  barabara ambayo  imekwanguliwa lami  na inafanyiwa ukarabati mpya kutokana na kutanda kwa vumbi eneo hilo na mwendo kasi wa mabasi hayo kuliweza kusababisha ajali kwa kushindwa kuonana na hatimaye kugongana uso kwa uso na watu sita kufariki papo hapo na mwingine kufariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya bunda .

kuhusu majeruhi wa ajali hiyo alisema majeruhi  wanne kati 14 ambao walikuwa hawajitambui wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya bugando kwa matibabu zaidi kwani hali zao sio nzuri kutokana na kuvuja damu nyingi na hivyo hospitali ya wilaya ya bunda kutokidhi mahitaji ya damu .

katika ajali hiyo  wanaume 27  na wanaume 20 wamejeruhiwa  ambapo majina ya miili ya marehemu  yamehifadhiwa kwaajili ya utambuzi  wa ndugu .


'' madereva wanashangaza sana kila mara tunaongea kuhusu mwendo kasi wa magari unaua lakini wao hawasikii  chelewa lakini ufike salama  ,haraka haraka haina  baraka ''alisema  mwakyoma.

baadhi ya abiria walikuwemo kwenye mabasi hayo walisema kuwa mabasi hayo yalikuwa na mwendo mkali ambapo walijaribu kupiga kelele kuwaambia madereva kupunguza mwendo lakini hawakuweza kusikilizwa na muda mfupi ajali ikatokea.

walisema kuwa ni vema sasa serikali ikachukua hatua kali kwa madereva wazembe ili kuzinusuru roho za watu ambao ni nguvu kazi ya taifa ambazo zinateketezwa kwa uzembe wa madereva.
 ..................................................................................................................................
 


Wanajeshi wa Ufaransa wanasema waasi wangali wanaudhibiti mji wa Konna
 
Maafisa katika jeshi la Ufaransa, wamekanusha madai yaliyotolewa awali na jeshi la Mali, kuwa wameweza kuudhibiti mji wa Konna uliokuwa umetekwa na waasi.
Ufaransa, ilianza harakati zake za kijeshi kusaidia jeshi la Mali dhidi ya waasi Ijumaa iliyopita baada ya wapiganaji wa kiisilamu kuuteka mji wa Konna na kuanza kuukaribia mji mkuu.
Mji mwingine wa Kati ,Diabaly, ulitekwa na waasi Jumatatu iliyopita.
Wanajeshi wa Ufaransa wakishirikiana na wa Mali, wameanza kuelekea katika mji huo kuanza operesheni yao ya ardhini dhidi ya waasi.
Mwezi Machi mwaka jana wapiganaji wa kiisilamu wakishirikiana na waasi wa Tauareg, waliteka Kaskazini mwa Mali.
Hivi karibuni wapiganaji hao walio na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda, walidhibiti eneo hilo na kuanza kuweka sheria kali za kiisilamu.
Pindi mpango wa serikali wa kuutwaa mji huo , waasi nao wakaanza kuelekea Kusini mwa nchi.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, alisema kuwa Ufaransa ina lengo moja tu, kuhakikisha inaondoka Mali, baada ya nchi hiyo kuwa salama na kuhakikisha kuwa hakuna tisho lengine la kigaidi dhidi ya nchi hiyo.
Hatua ya wanajeshi kuteka mji muhimu wa Konna wiki jana , ndiyo ilichochea Ufaransa kuchukua hatua za kijeshi kusaidia Mali.
Ndege za Ufaransa, zilianza kufanya mashambuliziya angani dhidi ya wapiganaji hao siku iliyofuata hadi Jumamosi.
Maafisa walisema kuwa jeshi la Mali lilisema limeweza kudhibiti mji wa Konna na kwamba wapiganaji
100 waliuawa.

Lakini waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian, aliambia waandishi wa habari mjini Paris kuwa mji huo bado uko mikononi mwa waasi.
Ndege za kijeshi za mali ziliweza kuzuia waasi waliokuwa wameingia eneo lililo katikati mwa miji ya Douentza na Gao.
Duru hata hivyo zinaarifu kuwa jeshi la Mali halina uwezo mkubwa wa kudhibiti waasi kivyao
 
 
 
 

Friday, January 11, 2013

UFARANSA TAYALI KUTOA MAJESHI YAKE MALI


Maandamano ya wananchi wanaotaka usalama Mali 

Wapiganaji wa Mali walioteka mji mwingine mpya wa Konna


Rais wa Ufaransa Francois Hollande, amesema nchi yake iko tayari kusaidia jeshi la Mali 
kupambana na waasi wanaodhibiti Kaskazini mwa nchi.
Amesema kuwa ataweza kujibu haraka ombi kwa serikali yake la kutoa msaada wa kijeshi kwa nchi hiyo ili kusitisha harakati za wapiganaji hao.
Lakini alisema kuwa wataweza tu kufanya kazi yao ikiwa Umoja wa Mataifa utawaidhinisha. Umoja wa Matifa hata hivyo ndio umetoa wito wa kupelekwa kwa wanajeshi wa kimataifa nchini humo katika mkutano wa dharura wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Rais Hollande, alisema kuwa harakati za wapigajani hao wanaohusishwa na kundi la Al Qaeda,sasa zinatishia utahbiti wa Mali. Hadi sasa Ufaransa imesema iko tayari tu kutoa mafunzo kwa jeshi la Mali.
Awali baraza la usalama la Umoja wa mataifa lilitoa wito wa kupelekwa kwa wanajeshi wa kimataifa nchini humo ambako wapiganaji wa kiisilamu wanadai wameuteka mji muhimu wa Konna.
Wakati huohuo, duru za kidiplomasia zinasema kuwa rais wa nchi hiyo ametoa wito kwa Ufaransa kusaidia katika kupambana na wapiganaji hao, hoja iliyojadiliwa katika mkutano wa dharura wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice, alihoji ikiwa rais Dioncounda Traore alikuwa ametoa ombi maalum na kufafanua aina ya msaada anaotaka.
Wapiganaji wa Mali walioteka mji mwingine mpya wa Konna
Mwezi jana Umoja wa Mataifa uliidhinisha mpango wa kutuma wanajeshi elfu tatu kuweza kutwaa eneo la Kaskazini mwa nchi ambalo linadhibitiwa na makundi ya kigaidi yaliyo na uhusiano na kundi la Al Qaeda.
Wapiganaji wa kiisilamu wameweka sheria kali za kiisilamu katika eneo hilo.
Kwa sababu ya mipango ya usafiri na vifaa , kikosi cha wanajeshi wa Afrika hakitatarajiwa kuanza kazi hadi ifikapo Septemba au Oktoba.
 .........................................................................................................

Waasi Jamuhuri ya Afrika ya Kati wasitisha vita

 

 
 
Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Francois Bozize akiwahutubia waandishi wa habari

Kiongozi wa waasi wa Seleka


Waasi wanaopambana na serikali katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wanasema kuwa wamekubaliana kusitisha mapigano kwa wiki moja baada ya mazungumzo ya amani nchini Gabon.
Waasi wanasema kuwa wanataka wanajeshi wa Afrika Kusini waondoke nchini humo na pia serikali iwaachilie wafungwa wa kisiasa ili waweze kuafikia mwafaka wa pamoja.
Waasi hao wa 'Seleka' walidhibiti maeneo ya Kaskazini na Mashariki kwa CAR katika kipindi cha wiki nne kuanzia Disema mwaka jana.
Wanamtuhumu rais Francois Bozize kwa kukiuka mikataba kadhaa ya amani ambayo walitia saini.

''Tutakubaliana kimsingi kutopigana kwa wiki moja'' alisema msemaji wa kundi hilo, Florian Ndjadder.

Aliongeza kuwa mwafaka utaweza kuruhusu waasi kuona ikiwa serikali itaweza kujitolea kupata suluhu kwa mzozo huu na kutimiza matakwa yao.
Waasi hao ambao wamekuwa wakimtaka rais kujiuzulu, pia walisema kuwa wanataka waziri mkuu mpya kuteuliwa kutoka kwa upinzani na hata kutoa madai zaidi.

" Mamluki hao kutoka Afrika Kusini lazima waondoke Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wafungwa wa kisiasa lazima waachiliwe bila vikwazo wakati huohuo,'' alisema bwana Ndjadder.
Afrika Kusini imeanza kutuma wanajeshi 400 kusaidia kudhibiti hali katika Jamuhuri ya Afrika ya kati. Wanajeshi kutoka nchi jirani pia wameweza kutumwa huko. Ufaransa na Marekani wamekataa ombi la serikali kusaidia katika kupambana na waasi hao
......................................................................................................
 

Bunge jipya lililokarabatiwa kwa zaidi ya dola milioni kumi
Wabunge nchini Kenya wamejizawadia

Wabunge nchini Kenya wamejizawadia dola 107,000 kama marupurupu katika mojawpao ya vikao vyao vya mwisho vya bunge hilo kabla ya uchaguzi mkuu kufayika mwezi Machi.
Kila mbunge ataweza kupata mlinzi wa maisha, pasi ya kidiplomasia na kupata huduma za juu zaidi katika viwanja vye ndege kote duniani. Haya ndiyo mapendekezo yaliyo katika mswaada waliopiitisha ukisubiri kuidhinishwa na rais Mwai Kibaki
Ni mara ya pili wabunge wamepitisha mswaada huu wa kujizawadia mwishoni mwa vikao vyao vyabunge . Rais Mwai Kibaki alitupilia mbali mswaada wa kwanza kama huu ambao ulizua ghadhabu miongoni mwa wananchi.

Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wabunge wanaopokea mishahara ya juu zaidi barani Afrika kila mmoja akipata dola elfu kumi na tatu kila mwezi.
Lakini mshahara wa mkenya wa kawaida ni takriban dola 1,700 kila mwezi.
Mswaada huu, ulipitishwa siku ya Jumatano na wabunge chini ya thelathini waliokuwa bungeni. Walikarabati bunge lao kwa kutumia dola milioni kumi na mbili kulingana na stakabadhi za bunge zilizotolewa hapo jana.

Malipo haya ni sawa na yale yaliyokuwepo katika mswaada walioupitisha mwezi Oktoba, lakini wakati huu wabunge hao pia wamependekeza marupurupu kwa rais ambaye atalipwa dola laki tatu sawa na makamu wa rais na waziri mkuu.

Alipotupilia mbali mswaada wa kwanza , Rais Kibaki lisema kuwa haiwezekani kwa wabunge kulipwa mamilioni ya dola wakati uchumi ungali umedumaa.
Tume ya kushughulikia mishahara ya wafanyakazi wa umme, iliambia wakenya kuwa hakuna uhakika ikiwa hatua yao inakuika katiba.

Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yameelezea kukerwa sana na hatua ya wabunge. Tayari waziri mkuu Raila Odinga amepinga mswaada huo akisema kuwa ni kama uhalifu dhidi ya wakenya na kwamba anashauriana na rais Mwai Kibaki kuhusu hatua itakayokuwa sawa kwa wakenya. 
.......................................................................................................
 



Monday, January 7, 2013

MAZIKO YA ANASTAZIA NDOBO NYUMBANI KWAKE MUSOMA

vitukuu na wajukuu wakiongoza kuingia eneo la maziko

mwili wa marehemu anastazia ndobo katika jeneza


wakati wa sala ya maziko


mahala alipozikwa nyumbani kwake kwangwa musoma mara




majonzi na huzuni vilitawala wakati wa salam za mwisho huyo ni mtoto wa marehemu


kabulini

ndugu jamaa familia wanaukoo majilani katika picha


mwili ukiwekwa kabulini


balozi ndobo akiweka mchanga katika kabuli la mkewe anastazia

mke mdogo akimuaga mwenzake

mama maria nae akiweka mchanga

wajukuu wakiweka mchnga

LALA SALAMA MAMA NDOBO

balozi ndobo na mke mdogo wakiweka mauwa

alikuwa rafiki mkubwa wa mama maria nyerere na aliweka shada la mauwa

watoto na wakezao wakiweka shada la mauwa

wajukuu wa wa marehemu

mtoto mkubwa wa marehemu akiteta jambo na mshereheshaji


ukoo wa anastazia ukiweka shada la mauwa

 
MENEJA WA HUDUMA KWA JAMII WA NHC MUUNGANO SAGUYA AKIZINDUA VYOO HIVYO
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limetoa msaada wa ujenzi wa jengo la vyoo lenye matundu 14 katika Shule ya Msingi Mwisenge aliyosoma Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni sehemu ya maazimisho ya Miaka 50 ya Shirika hilo.

Katika hotuba yake ya uzinduzi wa Jengo hilo uliofanyika shuleni hapo,Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika hilo Muungano Saguya alisema Shirika la nyumba la Taifa kwa kutamba wajibu wake kwa Jamii linayo sera ya kusaidia Maendeleo ya Jamii katika Nyanja mbalimbali.

Alisema licha ya kuwepo changamoto mbalimbali katika Shule hiyo yenye historia kubwa katika Taifa la Tanzania wamejaribu kupunguza changamoto hizo kwa kubolesha miundombinu ya vyoo ambayo imeghalimu kiasi cha shilingi milioni 16 ili kuviweka katika hali ya kuridhisha.      

Saguya alisema ili mtoto aweze kupenda shule pamoja na masomo ni wajibu kumuwekea mazingira mazuri ambayo yatamfanya kila wakati atamani kwenda shuleni na kujiepusha na utoro ambao unaweza kuzolotesha elimu.

“Kila mmoja wetu anafahamu kuwa ili Nchi yoyote iendelee inahitaji elimu kwa watu wake,Taifa letu halikadharika limekuwa likijitahidi kuwekeza katika elimu ili kuweza kwenda sambamba na mabadiliko makubwa ya uchumi na teknolojia ya Dunia.

“Hivi sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki tumeungana na Nchi jirani katika Nyanja za kiuchumi,hivyo itoshe kusema hatuwezi kushindana na Nchi hizi jirani kama tutapuuzia kuweka mkazo katika kuwekeza zaidi katika Elimu,”alisema Saguya.

Alisema NHC ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mahala pazuri pa kujistiri imeona itengeneze vyoo vya kisasa katika shule hiyo kwa kuwa shule isipokuwa na vyoo imara huwafadhaisha na kuwadhalilisha wanafunzi wengi.

“Shirika lina kila sababu ya kuenzi mchango wa Mwalimu Nyerere kama mnakumbuka NHC lilikuwa Shirika la kwanza kuanzishwa na Mwalimu Mwaka 1962 ikiwa ni Mwaka mmoja baada ya Uhuru.

“Mwalimu Nyerere alithamini sana vitu vitatu katika kuleta utu wa Mwanadamu vitu ambavyo ni pamoja na nyumba,mavazi na malazi hivyo tunatoa mchango huu kama shemu ya kuadhimisha miaka 50 na kuenzi jitihada za Mwalimu Nyerere la kulianzisha Shirika hili,”aliongeza.

Katika taarifa iliyotolewa na Meneja NHC Mkoa wa Mara Jocton Matogo juu ya ujenzi huo alisema ujenzi ulianza julai 2012 na kukamilika oktoba 2012 ikiwa na matundu saba kwa Wasichana na matundu saba kwa wavulana.  

Alisema  mradi wa choo cha wanafunzi katika shule hiyo uliibuliwa na uongozi wa Shirika Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na uongozi wa shule baada ya kutathimini mahitaji ya haraka na kutimiza sehemu ya miradi ya huduma ka Jamii inayotolewa na Shirika hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo Mathias Buguti amelishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa msaada waliotoa katika shule hiyo kwa kuwa ilikuwa ni hitaji lao kubwa kwa sasa kwa kuzingatia wingi wa wanafunzi katika shule hiyo
.
  


Saturday, December 29, 2012

MAUAJI YA BODABODA

MADEREVA WA PIKIPIKI WAKIPITA KATIKA BARABARA YA MKENDO KWENDA KUMSHUHUDIA MWENZAO HOSPITALI YA MKOA WA MARA

SEHEMU YA MGUU AMBAO PIA ULIKATWA NA MAPANGA  

BODABODA WAKIWA NJE YA HOSPITALI YA MKOA WA MARA

MWENZAO ACHINJWA


Mbunge atangaza vita na Nyani waharibifu

          -Mwananchi atakayeua nyani na kumpelekea mkia kulipwa elfu kumi



Mbunge wa Jimbo la Kibara Kangi Lugora (CCM) ametangaza vita na Nyani ambao amedai wamekuwa wakiharibu mazao ya Wananchi mashambani na wengine kuwadhuru watu katika maeneo yao ya makazi na kupelekea kukwamisha shughuli za kiuchumi zinazofanywa na Wananchi katika Jimbo hilo.

Akizungumza na BLOGU HII Mjini Bunda Kangi alisema tayari walishatoa taarifa Serikalini kupitia Wizara ya Mali Asili na Utalii kuhusiana na uharibifu unaofanywa na Nyani hao lakini wamekuwa kimya bila kuchukua hatua zinazostahili hivyo amaeamua kuwahamasisha Wananchi katika Jimbo lake kuhakikisha wanawaangaamiza Nyani wote katika maeneo yao.

Alisema nyani hao wamekuwa wakifanya uharibifu mkubwa ambao wameshindwa kuuvulia wakati walishatoa taarifa katika sehemu zinazohusika na kukaliwa kimya hivyo wameamua kwa nguvu zao kuhakikisha wanapambana na nyani hao na kuwaondoa kabisa katika maeneo yao.

Mbunge huyo alisema amewaajili watu watano ambao wanatumia siraha za bunduki na kijadi kuhakikisha popote wanakutana na nyani  kuwaua ili wasiendelee kuharibu mazao ya Wananchi na kuwadhuru binadamu kwa kuwa Serikali imeshindwa kulichukulia hatua suala hilo.

Alisema licha ya kuwaajili watu hao pia amewatangazia ajira Wananchi wa Jimbo hilo kwa yeyote atakaye ua nyani na kisha kumpelekea mkia atapewa shilingi elfu kumi papo hapo kwa kuwa amewaweka mawakala ambao wanatumia stakabadhi ambazo zimeandaliwa kwa kazi hiyo ya kuwalipa Wananchi.

"Hatuwezi kuendelea kukubaliana na hali hii ya kuharibiwa mazao yetu huku Serikali imekaa kimya tutawaua nyani wote kwa kuwa hawana faida kwetu na nimeshaandaa fedha za kutosha ambazo kila Mwananchi atakayefanya kazi hiyo atapata malipo yake,"alisema Kangi.

Alisema nyani hao wamekithiri sana katika milima ya Lagata,Ilamba na Kitengere ambapo amedai huko kote amewaweka mawakala ambao watahakikisha kila Mwananchi atakayepeleka mkia wa nyani anapata malipo yake papo hapo pasipo usumbufu.

"Kwanza nyani hawa sio utalii kwetu na hakuna mtu yeyote anayekuja hapa kufanya utalii wa kuangalia nyani na kama Serikali ingeona wanafaa kwa utalii wangesikiliza vilio vya Wananchi kutokana na adha wanayoipata ya kuharibiwa mazao yao na kuwadhuru Wananchi,"alisema Mbunge huyo. 

Mbunge Kangi aliongeza kuwa licha ya uharibifu wa nyani hao lakini pia kumekuwepo na matukio ya Wananchi kudhuliwa na Mamba pamoja na Viboko katika Ziwa Victoria ambapo pia wameanzisha vita ya kuhakikisha wanawawinda mamba pamoja na viboko na kuwaua.

Alisema hadi sasa watu wanne wameuwawa na mamba pamoja na viboko huku Serikali ikikaa kimya hivyo wao wameamua kuanzisha mapambano ambayo yatawaangamiza mamba na vibiko wote ambao wamekuwa wakiwadhuru Wananchi. 

.....................................................................................................................................

    Profesa Muhongo aijibu CUF kuhusu mgawo wa umeme



WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesisitiza kuwa hakuna hoja ya mgawo wa umeme kwa sasa hapa Nchini kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kujipanga kutafuta vyanzo vingine vya uzalisha mbadala wa umeme kuliko kutegemea maji ili ifikapo Mwaka 2013 Tanzania iweze kupata umeme wa uhakika.

Kauli hiyo ameitoa Mjini hapa katika kikao kilichowashilikisha Vijana wa Manispaa ya Musoma kutaka kujua ni changamoto gani zinazopelekea Mji huo kukosa Maendeleo na kuzungummzia jinsi Shirika hilo linavyoendeleaa kufanya mabadiliko katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi na kupata umeme wa uhakika.

Alisema anapingana na maazimio yaliyotolewa na Chama cha Wananchi (CUF) katika Baraza lake Uongozi lilofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam na kueleza kuwa upo mgawo usio rasmi wa umeme ambao unapelekea kero kwa Wananchi na kukwamisha shughuli za kimaendeleo ambazo zinahitaji nishati ya umeme.

Profesa Muhongo alisema suala la kukatika kwa umeme kwa dakika mbili ama tatu sio mgawo kama inavyoelezwa na Chama hicho bali ni kutokana na miundombinu ambayo imechakaa ambapo kwa sasa Tanesco imeelekeza katika kufanya jitihada za kuibadilisha ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo.

''Sote tunafahamu miundombinu ya Shirika hili mingi imechakaa na inahitaji mabadiliko ambayo kwa sasa kwa asilimia kubwa inafanyiwa kazi hivyo inapelekea kuwepo na kero ya kukatika kwa umeme kwa muda furani lakini sio kila siku na huo sio mgawo wa umeme jamani tuache propaganda za kisiasa katika masuala mengine ya maslahi ya Taifa,"alisema Muhongo.

Alisema yeye akiwa kama Waziri mwenye dhamana ya umeme atamueleza Waziri Mkuu ama Rais iwapo kutakuwa na mgawo wa umeme lakini sio watu kusimama na kusema kuna mgawo kitu ambacho amekiita ni uzushi ambao unatumiwa na wanasiasa katika propoganda zao ambazo hazina tija kwa Taifa.

Alidai Tanesco inajipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana na tayari imeanza programu ya kusambaza umeme Nchi nzima katika Vijiji na Wilaya na kusema kazi hiyo inahitaji kupana ushirikiano katika kuifanukisha na kuomba kupata maoni kwa kila Mwananchi namna ambavyo anataka shirika hilo lifanye katika kuleta ufanisi tofauti na kipindi cha nyuma

Aidha Profesa Muhongo alisema zipo changamoto nyingine ambazo zinafanywa na watu wasio wazalendo kwa kuiba mafuta ya Transifoma pamoja na waya za umeme hali inayopelekea kujitokeza kwa matatizo ya kukatika kwa umeme ili kupisha mafundi kuweza kurekebisha na kurudisha umeme na kuwaomba Wananchi kuweza kutoa taarifa pale wanapoona mtu anataka kuhujumu shirika hilo.

Akizungumzia masuala ya kimaendeleo katika Mji wa Musoma,Waziri Muhongo aliwataka vijana wa Mji huo kuacha ubinafsi na kushirikiana katika kujitafutia Maendeleo na kubadilisha muonekano wa Mji huo na kusisitiza kujiepusha na kukalia siasa muda wote bali wajishughulishe na shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo.
 

.................................................................................................................................

                          Amuuwa mtoto kwa kumchapa fimbo


MKAZI mmoja wa kata ya Nyasho katika Manispaa ya Musoma aliyefahamika kwa jina la Yohana Msafiri (38) amemuuwa mtoto wake Veronica Yohana kwa kumchapa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake Desemba 23 na kupelekea kifo chake akiwa njiani kupelekwa hospitali baada ya kuzidiwa na maumivu.

Katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari,Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mara Absalom Mwakyoma  alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 usiku katika maeneo hayo ya Nyakato ambapo chanzo cha kuchapwa viboko kwa mtoto huyo na matatizo ya kifamilia.

Alisema mzaza wa Mtoto huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na tukio hilo ambapo amedai mara baada ya kukamilika kwa upelelezi mzazi huyo atafikishwa Mahakamani kuweza kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kutokana na tukio hilo Kamanda Mwakyoma amewataka wazazi kuangalia adhabu mbadala ambazo wanaweza kuwapa watoto pale wanapokuwa wanafanya makosa katika kuwafunza na sio kuwa na hasira ambayo inaweza kupelekea madhara mengine makubwa zaidi.

"Wazazi lazima waangalie adhabu mbadala ambazo zinapaswa kupewa watoto pale wanapofanya makosa maana kwanza ifahamike hawa ni watoto na yaale wanayoyafanya ni kutopkana na utoto wao hivyo iwepo busara katika kutaka kutoa adhabu kwa watoto wetu,"alisema Kamanda Mwakyoma.

Katika tukio lingine Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi Mkoani Mara alisema mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Gogogo anayekadiliwa kuwa na umri kati ya m,ika 40 na 45 mkazi wa Bunda aliyekuwa akiishi kata ya Nyakato Mshikamano katika Manispaa ya Musoma aliuwawa kwa kushambuliwa na kuchomwa moto kwa kudaiwa anahusika katika matukio ya ujambazi.

Kamanda Mwakyoma alisema Wananchi wanapomuhisi mtu anashiliki katika matukio ya uhalifu ni vyema kutoa taarifa Polisi na si kujichukulia sheria mkononi kwani hata kama mtuhumiwa anashiliki anapokamatwa anaweza kutoa taarifa ambazo zinaweza kuwapata watu wengine ambao anashiliki nao katika matukio hayo.

Alisema kujichukulia sheria mkononi ni kosa kwa mujibu wa sheria na atakaye kamatwa kutokana na kosa la kujichulia sheria mkononi atafikishwa Mahakamani kutokana na kosa hilo na kutoa tahadhari kwa Wananchi kuacha tabia hiyo kwani haifai na sheria hairuhusu kujichukulia sheria mkononi.

....................................................................................................................................