Wednesday, January 16, 2013

MAUAJI YA KINYAMA TARIME

MAMA AUA MTOTO WAKE WA MIEZI 11 TARIME ,ANYOFOA BAADHI YA VIUNGO VYA KE



JESHI la polisi katika kanda maalumu ya Tarime na Rorya, linamshikilia mwanamke mmoja Prisca Mwita (22), mkazi wa mtaa wa Nyamisangura mjini Tarime, kwa tuhuma ya kunyofoa baadhi ya viungo vya mtoto wake mchanga na kusababisha kifo chake..
Kamanda wa polisi katika mkoa wa Kipolisi wa Tarime na Rorya, kamishina msaidizi  Justus Kamugisha, amesema kuwa  tukio hilo limetokea januari 11, mwaka huu, majira ya saa 2:00 asubuhi nyumbani kwa mwanamke huyo eneo la mjini Tarime.

Kamanda Kamugisha amesema kuwa mwanamke huyo anatuhumiwa kuua mtoto wake Happy Anthony mwenye umri wa miezi 11, baada ya kumkata sikio la kushoto, kumnyoa nywele za upande wa kushoto, kumnyoa nyusi za jicho la kushoto na kumchuna ngozi ya kichwa sehemu ya kushoto.
Amesema kuwa majirani waligundua unyama huo na kutoa tarifa kwa viongozi wa eneo hilo na kwamba mwanamke huyo  anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kuanzia leo .
tukio hilo limehusishwa na  imani za kishirikina, kwani ni la ajabu kwa mama mzazi kufanya unyama huo kwa mtoto wake.
...................................................................................................................................
 
Kamanda wa polisi mkoa wa mara absalom mwakyoma akitoa taarifa ya ajali mbele ya waandishi wa habari .
mabasi mawili jana jumapili yamegongana uso kwa uso na wilayani bunda mkoani mara na kusababisha  vifo vya watu sita papo hapo na mmoja kufikiaa hospitali teule ya wilaya ya bunda na kufikia idadi ya maiti saaba huku watu 47 wakijeruhiwa vibaya.

akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi Absalom Mwakyoma alisema kuwa ajali hiyo ilitokea  majira ya saa 11jioni  katika kijiji cha nyatwari Tarafa ya Serengenti wilayani bunda  karibu na hifadhi ya taifa ya Serengenti mpakani mwa mkoa wa mara na simiyu  na kuhusisha mabasi mawili  ya mwanza coach T756AWT aina ya scania marcopolo mali ya Halfan Ahmed wa mwanza likitoka  musoma kuelekea mwanza jina la dereva halikufahamika inaelekea alikimbia  dereva huyo na basi T535 AJR aina ya scania marcopolo bestline  lililokuwa likitokea mwanza kuelekea sirari wilayani tarime.

Mwakyoma alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa mabasi hayo na madereva kutokuwa makini  ambapo yalifika katika eneo  barabara ambayo  imekwanguliwa lami  na inafanyiwa ukarabati mpya kutokana na kutanda kwa vumbi eneo hilo na mwendo kasi wa mabasi hayo kuliweza kusababisha ajali kwa kushindwa kuonana na hatimaye kugongana uso kwa uso na watu sita kufariki papo hapo na mwingine kufariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya bunda .

kuhusu majeruhi wa ajali hiyo alisema majeruhi  wanne kati 14 ambao walikuwa hawajitambui wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya bugando kwa matibabu zaidi kwani hali zao sio nzuri kutokana na kuvuja damu nyingi na hivyo hospitali ya wilaya ya bunda kutokidhi mahitaji ya damu .

katika ajali hiyo  wanaume 27  na wanaume 20 wamejeruhiwa  ambapo majina ya miili ya marehemu  yamehifadhiwa kwaajili ya utambuzi  wa ndugu .


'' madereva wanashangaza sana kila mara tunaongea kuhusu mwendo kasi wa magari unaua lakini wao hawasikii  chelewa lakini ufike salama  ,haraka haraka haina  baraka ''alisema  mwakyoma.

baadhi ya abiria walikuwemo kwenye mabasi hayo walisema kuwa mabasi hayo yalikuwa na mwendo mkali ambapo walijaribu kupiga kelele kuwaambia madereva kupunguza mwendo lakini hawakuweza kusikilizwa na muda mfupi ajali ikatokea.

walisema kuwa ni vema sasa serikali ikachukua hatua kali kwa madereva wazembe ili kuzinusuru roho za watu ambao ni nguvu kazi ya taifa ambazo zinateketezwa kwa uzembe wa madereva.
 ..................................................................................................................................
 


Wanajeshi wa Ufaransa wanasema waasi wangali wanaudhibiti mji wa Konna
 
Maafisa katika jeshi la Ufaransa, wamekanusha madai yaliyotolewa awali na jeshi la Mali, kuwa wameweza kuudhibiti mji wa Konna uliokuwa umetekwa na waasi.
Ufaransa, ilianza harakati zake za kijeshi kusaidia jeshi la Mali dhidi ya waasi Ijumaa iliyopita baada ya wapiganaji wa kiisilamu kuuteka mji wa Konna na kuanza kuukaribia mji mkuu.
Mji mwingine wa Kati ,Diabaly, ulitekwa na waasi Jumatatu iliyopita.
Wanajeshi wa Ufaransa wakishirikiana na wa Mali, wameanza kuelekea katika mji huo kuanza operesheni yao ya ardhini dhidi ya waasi.
Mwezi Machi mwaka jana wapiganaji wa kiisilamu wakishirikiana na waasi wa Tauareg, waliteka Kaskazini mwa Mali.
Hivi karibuni wapiganaji hao walio na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda, walidhibiti eneo hilo na kuanza kuweka sheria kali za kiisilamu.
Pindi mpango wa serikali wa kuutwaa mji huo , waasi nao wakaanza kuelekea Kusini mwa nchi.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, alisema kuwa Ufaransa ina lengo moja tu, kuhakikisha inaondoka Mali, baada ya nchi hiyo kuwa salama na kuhakikisha kuwa hakuna tisho lengine la kigaidi dhidi ya nchi hiyo.
Hatua ya wanajeshi kuteka mji muhimu wa Konna wiki jana , ndiyo ilichochea Ufaransa kuchukua hatua za kijeshi kusaidia Mali.
Ndege za Ufaransa, zilianza kufanya mashambuliziya angani dhidi ya wapiganaji hao siku iliyofuata hadi Jumamosi.
Maafisa walisema kuwa jeshi la Mali lilisema limeweza kudhibiti mji wa Konna na kwamba wapiganaji
100 waliuawa.

Lakini waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian, aliambia waandishi wa habari mjini Paris kuwa mji huo bado uko mikononi mwa waasi.
Ndege za kijeshi za mali ziliweza kuzuia waasi waliokuwa wameingia eneo lililo katikati mwa miji ya Douentza na Gao.
Duru hata hivyo zinaarifu kuwa jeshi la Mali halina uwezo mkubwa wa kudhibiti waasi kivyao
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment