Friday, October 5, 2012

ZIWA VICTORIA NIKIVUTIO MUSOMA


unapokuwa musoma mjini ususani maeneo ya makoko seminari ndiyo unaweza kutazama jinsi ziwa linavyo onekana vizuri, kwambali nimajali ya mawe ambapo juu kunamnala ambao uliwekwa tokea enzi za utawala wa hawamu ya kwanza wakati bandali ya musoma ilipo kuwa inatumika kwa meli za mizigo na abilia lakini sasa hivi bandari hiyo ni sehemu ya popo,pimbi,njiwa na mapango ya wahalifu, kwenye mlima huo kulikuwa kuna taa nyekundu huwaka usiku ili kuiongoza meli kama ikiwa inatokea mwanza,kampala au kisumu sasa hivi hata mnala wenyewe sidhani kama hupo.

vilevile kwaupande wa kulia ukiwa maeneo hayohayo ya makoko beach utakiona kiwanda kikubwa sana cha minofu ya samaki wanaovuliwa katika ziwa hilo na minofu yake kuuzwa ulaya nikiwanda cha mwekezaji kutoka kenya kinajulikana kwa jina la BUKANGA bado kinaendelea kufanya kazi japo kwa kusuasua sidhani kama kinatoa huduma zamani.


hapo sio polini ni kisiwa cha RUKUBA BEACH ambapo kuna hotel ya kitalii iliyo jengwa zamani kidogo kuna ndani yake kuna vijiji kadhaa kuna Rukuba ndago ambapo pamoja na kuwepo mwekezaji na hotel hiyo pia wakazi wa hapo ni wavuvi wa dagaa na samaki sato na sangara wanao letwa kiwandani bukanga kila siku, kuna rukuba centani na hesaru wavuvi wengi utokea huko.


kiwanda cha samaki BUKANGA.


Dagaa wanao vuliwa na wakazi wa maeneo hayo ya MAKOKO BEACH huanikwa kila siku alfajili na jioni kuwekwa kwenye majunia kwaajili ya safari ya Dar,Arusha,Tunduma na nk dememja sh 3000 adi sh 5000 kutokana na hali yahewa itakavyo kuwa.



No comments:

Post a Comment