Tuesday, October 16, 2012

WAJUMBE WA CCM MWANZA WAPATA AJALI LEO



Wajumbe wa ccm wilaya ya misungwi leo hii wamepata ajali maeneo ya buhongwa iliyopo katika wilaya nyamagana walipo kuwa wakielekea katita uchaguzi mkuu ngazi ya mkoa wa mwanza majira ya saa 3.00 za asubuhi ambapo deleva wa basi hilo amepoteza maisha hapo hapo na wajumbe takriban saba nimajelui wako katika hospitali ya bugando kwa matibabu zaidi.


chanzo cha ajali hio ni basi hilo lilikuwa likikwepa loli aina ya fuso ambalo lilikuwa likigeuka kujiweka sawa kuingia barabarani  ndipo basi hilo likiwa katika mwendo kasi liligoga fuso na kupinduka papo hapo,wajumbe hao walikuwa safarini jijini mwanza katika uchaguzi wa wajumbe wa halmashauri kuu ya ccm mkoa wa mwanza unaofanyika leo katika uwanja wa ccm kirumba.

No comments:

Post a Comment