NA CALESI KATEMANA-MUSOMA.
MKAZI mmoja Ryoba David 39 wa kijiji cha Makutano wilaya ya Musoma amekatwa mguu wake wa kushoto baada ya kugongwa na pikipiki aina ya Bajaji Julai 1mwaka huu.
Akiongea na waandishi wa habari katika wodi namba 8 katika hospital ya mkoa wa Mara alikolazwa,David amesema kuwa baada ya kupata ajali hiyo alipelekwa katika hosptali ya mkoa wa Mara ambako alilazwa kwa muda wa siku mbili na kisha akahamishiwa katika hosptali ya rufaa Bugando kwa matibabu zaidi.
Alisema kuwa alipofika katika hospital hiyo ya rufaa Bugando alikutana na mgomo wa madakitari ambapo huduma zilikuwa si za kuridhisha kutokana na mgomo huo na kwamba alikaa huko kwa muda wa mwezi mzima huku huduma zikiwa za kusuwasuwa hali iliyosababisha mguu wake kuoza.
David alifafanua kuwa baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya aliamua kurudi katika hosptali ya mkoa wa Mara tarehe 13 mwezi huu na madaktari walipomuona waligundua kuwa mguu wake ulikuwa tayari umeshaoza hivyo waliamua kumkata,
‘’Kwakweli nilipofika hapa baada ya madkatari kuniona waliniambia kuwa mguu wangu huu umeshaoza na kwamba hakuna njia nyingine tofauti na kuukata ndipo tarehe 14 mwezi huu waliponikata kwakweli mimi nasikitika sana maana kilichochangia mimi kutopata huduma ni huu mgomo wa Madktari.’’alisema David kwa masikitiko makubwa.
Aidha alisema kuwa kama kusingekuwepo na mgomo huo huenda angeweza kupata huduma safi lakini kutokana na mgomo huo madktari waliokuwa wakipita katika wodi alilokuwa amelazwa walikuwa wakimuanagalia tu bila kumpa huduma yeyote.
David ameongeza kuwa anamushukuru mungu kwa vile yuko hai na kwamba anatarajia kununua mguu wa bandia ambao utamuwezesha kufanya kazi zake kama walivyo walemavu wengine .
Mwisho
No comments:
Post a Comment