Friday, August 31, 2012

Thursday, August 30, 2012

Kichekesho cha leo

kichekesho cha leo

Mama kapanda daladala na mwanae wa miaka miwili pembeni kakaa na njemba moja
Mama:nyonya basi mwanangu
Mtoto:anatingisha mabega kumaanisha hataki
Mama:Au nimpe anko
Mtoto:analia sitaki anadaka nyonyo anaendelea
punde si punde akaacha tena kunyonya
Mama:ntampa anko kama hautaki
Mama:nimpe
Njemba:ahaaaa mama kuwa na msimamo basi nshapitiliza vituo vitatu kama unanipa nipe au kama vipi nishuke kituo kinachofuata
Mama:haaah anko uko serious..?

Michezo

udisha harudi nyumbani hadi msimu uishe


David Rudisha
Mwanariadha wa Jamaica Yohan Blake anatumaini la kutenda maajabu atakaposhiriki mbio za Diamond League mjini Zurich siku ya Alhamisi.
Alipokimbia mjini Lausane wiki iliyopita katika mbio za mita 100 aliweka mda mzuri ila tu Bolt ndiye ana mda bora kuliko.
Blake, aliyeshinda medali za fedha katika mbio za mita 100 na 200 wakati wa Olimpiki ataongoza orodha ya washindi wa medali za dhahabu 15 mjini London 2012.
Hata hivyo bingwa huyu wa Dunia hatoshindana na Bolt baada ya kukubaliana kuwa hawatoshindana baina yao kwa kipindi cha msimu kilichosalia. Bolt ana mipango ya kukimbia mita 200 kwenye uwanja wa mjini Zurich wa Letzigrund.
Blake, aliyeingia msimu huu akiwa na mda wa 9.82 kutoka mashindano ya Zurich ya mwaka jana aliweka mda mzuri msimu huu wa 9.75 kabla ya kunyoa sekunde nyingine huko Lausanne na kuweka sekunde 9.69 mjini Lausanne, hapo kesho atashindana na Tyson Gay pamoja na Ryan Bailey wote wa Marekani.
Mshindi wa medali sita za Olimpiki Usain Bolt, aliyeweka mda wa sekunde 19.58 mjini Lausanne atapambana na mwananchi mwenzake Warren Weir, aliyeshinda medali ya shaba kwenye Olimpiki za London na vilevile Jason Young.
Kwingine David Rudisha, aliyevunja rekodi ya mbio za mita 800 duniani kabla ya kushinda medali ya dhahabu mjini London atashiriki mashindano pekee kufuatia mashindano ya Olimpiki mjini London.
Rudisha ambaye tangu wakati huo hajarudi nyumbani ana imani ya kuweka mda mzuri.
Alielezea sababu yake ya kutorudi nyumbani kama kutaka kujiweka katika hali ya ushindani bila kupoteza mazowezi, Lau kama ningekwenda nyumbani ningewekwa katikati ya vivutio ya sherehe na nisahau kua kuna mazowezi." Rudisha aliiambia BBC. "kwa hiyo ilibidi nikae Ulaya kuhitimisha msimu kisha nitarudi nyumbani nishe
Habari hii kwa hisani ya idhaa ya kiswahili ya BBC

DUNIA IMEPUUZA HALI YA MALI



Hali ya njaa nchini Mali
Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa wa haki za binadamu Valerie Amos amesema kuwa dunia imeshindwa kuwajibikia hali ya hatari kwa usalama wa raia wa Mali, ambako zaidi ya watu nusu milioni wametoroka makwao kutokana na vita.
Bi Valerie Amos, ambaye amekuwa akizuru kambi za wakimbizi ametoa wito wa msaada zaidi na ufadhili kuongezwa baada ya jamii ya kimtaifa kukusanya tu nusu ya pesa zinazohitajika kukabiliana na hali nchini humo.
Bi Amos yuko katika ziara ya siku tatu nchini Mali kujionea hali na athari za mzozo baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi.
Tangu hapo, wapiganaji wa kiisilamu wa kabila la Tuareg wameteka maeneo ya kaskazini mwa Mali.
Mwandishi wa BBC David Loyn, ambaye yuko katika msafara wa Amos, anasema kuwa mzozo huo umeathiri pakubwa nchi hiyo na kufanya rasilimali kuwa dunia kabisa.
Juhudi za kutoa msaada katika eneo la kaskazini zimeathirika kutokana na mapigano.
Bei ya juu ya vyakula pamoja na kipato cha chini zimesababisha hali ngumu kwa wananchi wa Mali.
Serikali mpya ya muungano, iliundwa katika mji mkuu Bamako,mwishoni mwa wiki ikiahidi kuleta mageuzi na utahibiti katika maeneo ya kaskazini mwa nchi.
Wapatanishi kutoka muungano wa nchi za magharibi ECOWAS, wamefanya mazungumzo na wapiganaji hao, na hata kupeleka wanajeshi elfu tatu nchini Mali ikiwa ni sehemu juhudi za amani hazitazaa matunda.
Wapiganaji wa Tuareg waliteka eneo la kaskazini baada ya rais Amadou Toumani Toure kupinduliwa mwezi Machi.


David Ryoba akiwa anahojiwa na Mwandishi wa habari Cales Katemana

Mmiliki wa baa ya Mazami ,David Ryoba akiwa anahojiwa na mwandishi wa habari  Cales Katemana  katika hosptal ya mkoa wa Mara  kuhusu ajali aliyoipata iliyosababisha akatwe mguu wake wa kushoto hivi karibuni-picha na Cales KatemanaAdd

MGOMO WA MADKITARI WASABISHA AKATWE MGUU



NA CALESI KATEMANA-MUSOMA.

MKAZI mmoja  Ryoba David 39 wa kijiji cha Makutano wilaya ya Musoma amekatwa mguu wake wa kushoto baada ya kugongwa na pikipiki aina ya Bajaji Julai 1mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari katika wodi namba 8 katika hospital ya mkoa wa Mara alikolazwa,David amesema kuwa baada ya kupata ajali hiyo alipelekwa katika hosptali ya mkoa wa Mara ambako alilazwa kwa muda wa siku mbili na kisha akahamishiwa katika hosptali ya rufaa Bugando kwa matibabu zaidi.

Alisema kuwa alipofika katika hospital hiyo ya rufaa Bugando alikutana na mgomo wa madakitari ambapo huduma zilikuwa si za kuridhisha kutokana na mgomo huo na kwamba alikaa huko kwa muda wa mwezi mzima huku huduma zikiwa za kusuwasuwa hali iliyosababisha mguu wake kuoza.

David alifafanua kuwa baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya aliamua kurudi katika hosptali ya mkoa wa Mara tarehe 13 mwezi huu na madaktari walipomuona waligundua kuwa mguu wake ulikuwa tayari umeshaoza hivyo waliamua kumkata,

‘’Kwakweli nilipofika hapa baada ya madkatari kuniona waliniambia kuwa mguu wangu huu umeshaoza na kwamba hakuna njia nyingine tofauti na kuukata ndipo tarehe 14 mwezi huu waliponikata kwakweli mimi nasikitika sana maana kilichochangia mimi kutopata huduma ni huu mgomo wa Madktari.’’alisema David kwa masikitiko makubwa.

Aidha alisema kuwa kama kusingekuwepo na mgomo huo huenda angeweza kupata huduma safi lakini kutokana na mgomo huo madktari waliokuwa wakipita katika wodi alilokuwa amelazwa walikuwa wakimuanagalia tu bila kumpa huduma yeyote.

David ameongeza kuwa anamushukuru mungu kwa vile yuko hai na kwamba anatarajia kununua mguu wa bandia ambao utamuwezesha kufanya kazi zake kama walivyo walemavu wengine .

Mwisho

nondo za onlinejournalism

.
wanahabari wakifurahia jambo kulia ni calesone na kushoto pascal wakiwa katika mapumziko